HOSTELI YA BILIONI 2.5 KUJENGWA CHUO CHA MICHEZO MALYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 23 January 2023

HOSTELI YA BILIONI 2.5 KUJENGWA CHUO CHA MICHEZO MALYA

Na Shamimu Nyaki

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii mwisoni mwa wiki Januari 2023 imefanya ziara katika Chuo Cha Michezo Malya kilichopo Kwimba Mwanza, kuona maendeleo ya  ujenzi wa Hosteli ya Wanachuo ambayo itagharimu kiasi Cha Shilingi Bilioni 2.5 hadi kukamilika.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Mhe. Stanslaus Nyongo ambaye pia ni Mbunge wa Maswa imepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi  wa  Hosteli hiyo kutoka kwa Meneja Mradi Bw. Chaguo Mghoma aliyeeleza kuwa, ujenzi wa Hosteli hiyo ni wa ghorofa nne, ambapo hatua ya kwanza itahusisha ghorofa mbili.

"Hosteli hii itakapokamilika itakua na uwezo wa kuhudumia wanachuo  takriban 192 ambapo hadi Sasa umefikia asilimia 26" amesema Bw. Mghoma.

Kamati hiyo pia imetembelea eneo litakalojengwa Kituo cha Kitaifa cha kukuza na kuendeleza michezo ambacho kitahusisha Viwanja vya michezo, bwawa la kuogelea lenye  hadhi ya Olimpiki, Hosteli, Jengo la Utawala, eneo la mazoezi pamoja na madarasa.

Lengo la kujenga Kituo hicho ni kuongeza wigo wa udahili wa wanachuo ili kuzalisha Wataalamu Bora wa michezo, ambapo walengwa wengi ni Wanafunzi watakaopatikana katika  shule 56 zilizotengwa kwa ajili ya michezo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hassan Abbasi na Viongozi wengine wa wizara wameshiriki.

No comments:

Post a Comment