Na
Faustine Gimu, Sengerema - Mwanza
RAI
imetolewa kwa Asasi za Kiraia zinazotekeleza Miradi ya afya katika Mkoa wa
Mwanza na Shinyanga kuendelea kuwa na desturi ya kufanya kazi kwa kushirikiana
na Halmashauri ili kushirikisha jamii katika uimarishaji wa huduma
bora za afya na kuleta mabadiliko chanya.
Rai
hiyo imetolewa Januari 30, 2023 Wilayani Sengerema mkoani Mwanza na
Mratibu wa Huduma za Afya katika jamii kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa [OR-TAMISEMI] Martha Mariki katika ufunguzi wa mafunzo ya
Tathmini Shirikishi ya Kijamii (Community Score Card) ambayo ni moja ya
Afua ya Ushirikishaji Jamii yanayoratibiwa na Wizara ya Afya, Idara ya
Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma, Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii kwa
kushirikiana na AMERICARES Kupitia Mradi wa UZAZI STAHA.
Martha
amesema ni muhimu, Asasi za Kiraia kushirikiana na Serikali katika
kuwezesha Maendeleo hususan Sekta ya Afya.
“Moja ya kitu ambacho tunakiamini ni Community
Empowerment, Usipoweza kufanya community Empowerment wananchi watakuwa tegemezi
badala ya wao kushiriki kufanya mambo fulani ya kuleta maendeleo na watakuwa
wanaisubiri serikali kupeleka huduma, hivyo sisi kama Asasi za Kiraia na
Serikali kwa ujumla ni muhimu kushirikisha jamii na itatupeleka pazuri kwa
maendeleo ya Sekta ya Afya” amesema.
Aidha,
Martha amesema ni muhimu kufanya kazi kama timu baina ya serikali na asasi
mbalimbali za kiraia ili kuleta ufanisi katika sekta ya Afya.
“Katika
Sekta ya Afya ukifanya kivyako bila kushirikiana na wengine ni rahisi sana
kufeli, lakini ukifanya kama timu tunajijengea imani kuwa tunaweza
kuifanya kazi yetu kwa uhakika na bila kuchosha akili, nia madhubuti ya
kushirikisha kundi hili la asasi za kiraia [CSO,s] nia yetu ni kutusaidia
kupeleka mafunzo katika halmashauri namna zinavyotoa mafunzo kwenye jamii,” amesema.
Kwa
upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya
Afya kwa Umma Orsolina Tolage amesema, serikali itaendelea kuandaa Miongozo ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Huduma za Afya ikiwemo afua hii ya
Tathmini Shirikishi ya Kijamii ambapo mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo
wawakilishi kutoka Asasi za Kiraia kuwa na mipango ya pamoja itakayosaidia
kuleta mabadiliko chanya na kuendelea kuboresha huduma za afya.
“Mafunzo haya yatawajengea uwezo namna gani
wataweza kutekeleza hatua za ushirikishaji jamii katika kutekeleza afua ya
ushirikishwaji wa jamii kutatua changamoto na kuweka mipango madhubuti ya
kuweza kutekeleza pale ambapo wanaona hapafanywi vizuri, mfano, kwenye vituo
ambapo wanapata huduma wananchi na tathmini shirikishi hii ya kijamii
inashirikisha wananchi kukaa kwa pamoja kujadili na kuweza kuweka mpango
mkakati wa namna ya kuiondoa ile changamoto ili waweze kuboresha huduma kwenye
vituo vyao,” amesema.
Ikumbukwe
kuwa Mafunzo hayo ya tathmini shirikishi ya jamii sekta ya afya yanatolewa
kwa asasi za kiraia kutoka mikoa ya Mwanza kwa halmashauri ya Magu, Sengerema, Ukerewe
na Misungwi na Mkoa wa Shinyanga kwa Halmashauri ya Msalala, Kishapu na
Manispaa ya Shinyanga.
No comments:
Post a Comment