TPA WARAHISISHA MAMBO KWA WATEJA, WAJA KIDIJITALI ZAIDI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 22 December 2022

TPA WARAHISISHA MAMBO KWA WATEJA, WAJA KIDIJITALI ZAIDI...!

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Juma Kijavara akizunguza na wanahabari.

Na Joachim Mushi, Bagamoyo

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kuboresha huduma zake na kumrahisishia mteja inatarajia kuzindua kadi maalumu ya malipo 'Master Card' ambayo itamwezesha mteja kulipia malipo ya huduma za TPA moja kwa moja popote alipo kupitia kadi hiyo. 

Akizungumza na wanahabari Mjini Bagamoyo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Juma Kijavara amesema kadi hiyo itazinduliwa rasmi Desemba 30, 2022 ikiwa ni miongoni mwa maboresho ya huduma za TPA kwa wateja wake. 

"...Tunakwenda kuzinduwa kadi ya malipo, yaani Master Card ya TPA ambayo mteja wetu sasa atakuwa na uwezo wa kuweka hela katika kadi hiyo na kulipia tozo zetu moja kwa moja kupitia kadi hiyo."

Aliongeza kama hiyo haitoshi katika maboresho hayo watazinduwa pia App ya TPA inayokwenda kumrahisishia zaidi malipo kwa mteja wa TPA. Aliongeza kuwa kupitia App hiyo mteja ataweza kupata huduma za TPA moja kwa moja popote alipo na hata kufanya malipo pasipo kumlazimu kwenda benki. 

"...Kwa maboresho haya si lazima mteja wetu aende benki ataweza kupata huduma na hata kufanya malipo yake popote alipo," alisema Naibu huyo Mkurugenzi Mkuu wa TPA akizungumza ana wanahabari. 


No comments:

Post a Comment