| Wahitimu wa Mahafali ya Kwanza ya fani ya Ubaharia yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA), wakiwa kwenye hafla ya mahafali yao jijini Dar es Salaam. |
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya mapinduzi makubwa katika kuboresha usafiri wa majini kwa kujenga meli na kusomesha wataalam anuai wa fani ya bahari.
Akizungumza katika mahafali ya
kwanza ya kozi ya ubaharia ambayo yamefadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati
(CCTTFA) jijini Dar es Salaam amewataka wahitimu wa kozi hiyo, kuwa na nidhamu
ili ujuzi walioupata uwe na manufaa kwa taifa na nchi za ushoroba wa kati kwa
ujumla.
“Baharia mzuri ni yule mwenye
nidhamu anapokuwa akitekeleza majukumu yake, maono na anayezingatia usalama
wake, chombo na mali kwa ujumla,” amesisitiza.
Aidha amekitaka Chuo cha Bahari (DMI)
kuhakikisha kinakuza mtandao wake na taasisi mbalimbali duniani ili kuwawezesha
wanafunzi wa chuo hicho kupata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi ya vitendo
melini (Sea time).
Hata hivyo, Prof. Makame ameupongeza wakala wa
ushoroba wa kati kwa kuwafadhili wanafunzi hao na kuahidi kutilia mkazo wa kuwa
na mpango unaotekelezeka wa mafunzo kwa vitendo.
“Serikali tunajukumu kubwa la
kuhakikisha wanafunzi wetu wa fani za bahari wanapata mafunzo kwa vitendo ya
kutosha (Sea time) ili kuwaongezea ujuzi, kwenye utekelezaji wa kazi zao,”
Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Captain Dieudonne Dukundane ameipongeza Tanzania kwa kutumia rasilimali zake katika kuhakikisha wahitimu wa nchi zote za ushoroba wa kati wanasoma na kuhitimu salama, na kusisitiza wahitimu hao kuwa wazalendo na kufikia malengo ya kuhimarisha huduma za usafiri majini.
Amezungumzia umuhimu wa nchi Wanachama
wa Ukanda wa ushoroba wa Kati kutekeleza
program walizojiwekea za kuimarisha usafiri na usafishaji hususani katika
bahari na maziwa ili kukuza uchumi wa nchi zoo.
Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari
DMI, Dk. Tumaini Gurumo amesema wahitimu hao wamepata mafunzo stahiki
ambayo yatawawezesha kufanya kazi katika
nchi zote zenye bahari na maziwa duniani.
Pamoja na hayo amezungumzia umuhimu
wa kuwa na meli zinazomilikiwa na nchi wanachama wa ukanda wa ushoroba wa kati
ili kuimarisha mazoezi ya vitendo kwa mabaharia.
Jumla ya wanafunzi kumi kutoka nchi
wanachama wa Ushoroba wa Kati, ambazo ni Rwanda, Burundi, Uganda , DRC Kongonna
Tanzania.

No comments:
Post a Comment