| Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Meneja Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
| Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame
Mbarawa akiwa na wataalam wake akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara ya BRT
II toka Katikati ya Jiji – Mbagala KM 20.3, jijini Dar es salaam. |
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Prof. Mbarawa amesema katika kipindi cha miezi mitatu kutoka sasa anatarajia barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 20.3 itakuwa imefunguliwa yote kwa matumizi.
“Nia ya Serikali ni
kupunguza msongamano Dar es Salaam hivyo nakuagiza TANROADS na Mkandarasi
kuhakikisha sehemu inayokamilika magari yaruhusiwe kuitumia wakati ujenzi
unaendelea ili kupunguza msongamano na kuleta ufanisi katika huduma za usafiri
na uchukuzi katikati ya jiji la Dar es Salaam,” amesisitiza Prof. Mbarawa.
Aidha amewataka madereva wa magari katika barabara ambazo ujenzi wake bado unaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ili kulinda usalama wa abiria, wajenzi na magari kwa ujumla.
“…Hatuitaji ajali zitokee hivyo tutii maelekezo ya wataalam wetu yenye nia ya kupunguza msongamano na kulinda usalama wa watu na magari,” amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa Barabara na Magaraja jijini Dar es Salaam unafanywa kwa awamu hivyo wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali ili kufikia malengo tarajiwa yaliokusudiwa.
Kwa upande wake, Meneja
Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari amesema ujenzi wa Daraja la Juu sehemu ya
Chang’ombe makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa uko sahihi kulingana na
usanifu wake, lengo ni kutoa nafasi katikati kwa magari yaendayo haraka.
Amezungumzia umuhimu
wa raia wema kupata taarifa sahihi kwa
TANROADS pale wanapoona katika miradi hiyo kuna jambo linaloitaji
ufafanuzi.
Naye Mbunge wa Temeke,
Mhe. Doroth Kilave ameishukuru Serikali na kuipongeza Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi kutokana na kasi ya ujenzi wa miadi hiyo katika jimbo lake.
Takribani Shilingi Bilioni 262 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Barabara ya kupunguza msongamano ya Kilwa na Daraji la Chang’ombe katika makutano ya Barabara za Nyerere na Kawawa jijini Dar es Salaam.
| Taswira ya barabara ya Kilwa ambayo Ujenzi wake unaendelea katika makutano ya Barabara hiyo na ya Nelson Mandela Kurasini Jijini Dar es Salaam. |
| Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Meneja Mradi wa BRT, Eng. Barakaeli Mmari alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
| Muonekano wa Barabara ya Kilwa katika Makutano ya barabara hiyo na ya Nelson Mandela Kurasini Jijini Dar es Salaam ambayo ujenzi wake unaendelea. |
| Muonekano wa Barabara ya Kilwa na Daraja la Juu katika Makutano ya barabara hiyo na ya Nelson Mandela Kurasini Jijini Dar es Salaam ambayo ujenzi wake unaendelea. |

No comments:
Post a Comment