MUFTI WA TANZANIA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUFANYA DUA MAALUMU KUKABILIANA NA UKAME - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 5 November 2022

MUFTI WA TANZANIA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUFANYA DUA MAALUMU KUKABILIANA NA UKAME

Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi akihutubia hadhara iliyokusanyika katika Maulidi ya Manyema.

Na Dunstan Mhilu

MUFTI wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zuberi amewataka Viongozi wa dini na waumini wa Imani zote kufanya dua maalumu ili kukabiliana na ukame uliopo Nchini na Duniani kwa ujumla.

Rai hiyo ilitolewa juzi usiku na Kiongozi huyo wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania wakati wa maadhimisho ya kumbukizi ya Mazazi ya Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika katika Msikiti wa Manyema Dar es Salaam.

“Leo (juzi) nina maagizo kwa Masheikh, Walimu, Maimamu, Waumini wa Kiislam na ndugu zetu Wachungaji, Mapadre na wananchi wote kumuomba Mwenyezi Mungu atusamehe pale tulipoteleza atuondolee janga hili ambalo limezikumba nchi za Afrika Mashariki na sehemu nyingine za dunia, ukame huu siyo hapa tu juzi nilikuwa Comoro hali ni mbaya sana niwaombe tufanye dua ili Mungu atuepushie mbali dhoruba hii lazima kuna mahali tumekosea” alisema Mufti

Aidha alikemea baadhi ya maneno ya kupotosha umma yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa nchi imeingia kwenye ukame kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan kaanza vibaya, alisema kutamka maneno kama hayo ni kosa Rais hatoi baraka za kimungu aachwe afanye kazi ya kuwatumikia wananchi.

“Mambo kama haya yasipokemewa yanaleta taswira mbaya sisi wenyewe tujiulize wapi tulipojikwaa na tumrudie Mungu atunusuru na balaa hili ambalo linaangamiza Wanyama wetu, wakina mama nao wakikumbana na changamoto ya kusaka maji umbali mrefu huku miji mikubwa bei ikizidi kupaa naamini Mungu ni mwingi wa rehema anajibu unapomlilia lakini kama humuombi hawezi kukupa”

Vilevile aliipongeza serikali ya Rais Samia kwa amani na utulivu uliopo nchini na kuwataka waumini wajenge utamaduni wa kuwaombea viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wan chi.

Hata hivyo akizungumzia hadithi moja wapo ya Mtume Muhamad (S.A.W) aliwakumbusha waislam kuishika sana elimu, moja ya elimu hiyo ni kujenga utamaduni wakusoma Habari za Mungu na zile za kidunia.

“Popote utakapoiona elimu uichukie hiyo usiiache, elimu ni kitu ambacho muumini amepotelewa nacho na Mtume aliagiza tafuteni elimu na siyo kudharau suala la elimu, soma Quran yako ,jivunie kuwa Muislam lakini cha ajabu wapo waislam leo hii wanauponda uislam kwakufanya hivyo mnakosea,” alisema Muft.

Waumini wa dini ya Kiislam wanaendelea na maadhimisho ya kumbukizi ya Mazazi ya Mtume Muhamad (S.A.W).

No comments:

Post a Comment