Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba (kulia) na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania Mhe. Kim Sun Pyo, wakionesha hati ya mikopo nafuu ya jumla ya dola za Marekani bilioni moja sawa na shilingi trilioni 2.3 kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Korea (EDCF) kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil akizungumza baada ya aada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji saini mikopo nafuu ya jumla ya dola za Marekani bilioni moja sawa na shilingi trilioni 2.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
NA MUSSA KHALID,DAR ES SALAAM
Serikali
imesaini makubalino na serikali ya Jamhuri ya Korea mkopo nafuu wa Dola Bill 1
sawa na Tsh.Trilioni 2.3 kutoka mfuko wa ushirikiano wa kiuchumi wa Maendeleo
ya Korea (EDCF) kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Hafla
ya utiaji saini imefanyika leo jijini Dar es salaam baina ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emannuel Tutuba pamoja na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya
Korea Kim Sun Pyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba amesema kuwa baadhi
ya miradi ambayo itatekelezwa ni pamoja na Mradi wa Upanuzi wa Mfumo wa
Vitambulisho vya Taifa awamu ya pili ambao utagharimu Dola Mill 70 sawa na Bill
63.1 za kitanzania .
Aidha
amesema fedha hizo zitatumika katika uboreshaji wa miundombinu ya Taifa pamoja
na taarifa za ardhi kwa Dola za Kimarekani Mill 65 zawa na Bill 151.5 za kitanzania.
‘Miradi mingine ni wa uendelezaji wa Mifumo ya Usambazaji wa Majisafi na ya Kutibu majitaka kwa dola za Marekani milioni 70 sawa na sh. bilioni 163.1 na Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Kisasa cha mafunzo ya Usafirishaji wa Reli kwa dola za Marekani milioni 80 sawa na sh. bilioni 186.4’amesema Tutuba
Tutuba amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha ufanisi wa utekelezaji wa miradi yote iliyofadhiliwa kwa fedha za makubaliano haya zinatumika vizuri kufikia malengo yaliyokusudiwa
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania Kim Sun Pyo, amesema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wake.
Naye Katibu Mkuu
Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, ameishukuru
Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania kwa kuendelea kufadhili miradi mbalimbali nchini ukiwemo
Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar ambayo
inatarajiwa kuwa hospitali kubwa.
Hata hivyo Dkt. Akil amesema kuwa Ujenzi wa Hospitali ya Binguni utafungua fursa muhimu katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini kwa kuwa ni sekta muhimu katika nguvu kazi na maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment