DIASPORA ENDELEENI KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA - DKT. MPANGO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 20 September 2022

DIASPORA ENDELEENI KUCHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA - DKT. MPANGO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa `Tanzzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mageuzi katika sekta ya elimu ulioshirikisha Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Taasisi na Mashirika na wadau wa elimu jijini New York, Marekani tarehe 19 Septemba, 2022.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana na Diaspora wa Tanzania waliopo katika miji ya New York, Connect Cut na New Jesry nchini Marekani na kuwasihi kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Jijini New York alipokutana kwa mazungumzo na viongozi pamoja na wanajumuiya ya wanadiaspora hao Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Mpango amesema kitendo cha wanaDiaspora hao na wengine walioko duniani kote kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kinaendeleza jitihada za serikali za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wake.
 
''Muendelee kujishughulisha na shughuli za uwekezaji nchini kwani kufanya hivyo mnachangia maendeleo ya nchi yenu, mnaiunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo kwa watu  wake," alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia amewasihi wanadiaspora hao kufuatilia na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini kwa manufaa yao binafsi, ndugu na jamaa na Taifa lao kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango amewataka wanadiaspora hao kuendelea kutafuta na kushawishi wawekezaji wengi kuja nchini na kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazopatikana nchini na kuendelea kuisemea vizuri nchi yao ya Tanzania.

Amewapongeza Diaspora wa Tanzania kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa wa uwekezaji hasa kupitia mfuko wa UTT Amis ambapo aliasema kuwa hadi kufikia mwaka 2021 wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wamewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 3.9 za kitanzania katika mfuko huo.

No comments:

Post a Comment