KATIBU MKUU ELIMU DKT. FRANCIS AFUNGUA UMISSETA 2022 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Thursday, 11 August 2022

KATIBU MKUU ELIMU DKT. FRANCIS AFUNGUA UMISSETA 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael Agosti 10, 2022 wakati akifungua  Mashindano ya Michezo na  Sanaa kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) mkoani Tabora.

SERIKALI inakusudia kuongeza idadi ya Vyuo vya Elimu vinavyofundisha somo la michezo kufikia 6 kutoka vyuo 4 vya awali.

Hayo  yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael Agosti 10, 2022 wakati akifungua  Mashindano ya Michezo na  Sanaa kwa Shule za Sekondari (UMISSETA) mkoani Tabora, na  kusisitiza nidhamu na maadili kwa washiriki wa mashindano hayo.

"Maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyota Agosti 04, 2022 wakati anafungua mashindano haya, na ya mwaka (21) mkoani Mtwara  tumeyazingatia na tumeanza kuyafanyia kazi ikiwemo kuongeza idadi ya Vyuo vya Elimu viwili vya Tabora TTC na Mpwapwa TTC kufundisha somo la Elimu kwa Michezo" amesema Dkt. Francis.

Dr. Francis amempongeza Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele katika michezo na Sanaa, ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti katika Sekta hizo ambazo ni miongoni mwa Sekta ambazo zinatoa ajira kwa vijana.

Ameongeza kuwa, mashindano hayo pia itajumuisha Sanaa za jukwaani ikiwemo ngoma, Kwaya na Muziki wa Kizazi kipya, huku akitaka michezo hiyo kuendeshwa kwa kuzingatia maadili ya Taifa hilo.

Aidha, Dkt. Francis amesisitiza kuwa, mashindano hayo yanasaidia kukuza vipaji, kujenga upendo na kutoa fursa kwa Taifa kupata vijana watakaocheza katika timu mbalimbali za Taifa ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment