Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
JAMII imeaswa kuzingatia
suala la maadili kuweza kuzalisha watu watakao kuwa na uzalendo na nchi yao katika
kulinda, kutunza rasilimali za Taifa ikiwemo miundombinu ya mawasiliano ambayo ndiyo
kiungo muhimu katika nyanja ya usalama.
Hayo yamebainishwa na Afisa
Mkufunzi Mkuu Kiongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)
Dodoma, Bw. Faustine Malecha alipotembelea Banda la Shirika la Mawasiliano
Tanzania, TTCL katika maonesho ya Siku Kuu ya Wakulima yanayofanyika Kanda ya
Kati kwenye Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Bw. Malecha aliyeambatana
na Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaosomea Falsafa na Maadili
walioko katika mafunzo ya vitendo TAKUKURU Dodoma, ameipongeza TTCL kwa hatua kubwa
iliochukua kuhakikisha inarejesha huduma bora za mawasiliano kwa Watanzania.
Amesema mtazamo aliokuwa
nao kuhusu TTCL na baada ya kufika bandani hapo na kupokelewa vizuri na moafisa
waliotumia utaalam wao kuelezea shughuli kubwa zinazofanywa na shirika hilo, amebaini
kuwa kuna mabadiliko makubwa kimaendeleo ikilinganishwa na lilivyokuwa hapo awali.
Amesema TTCL ni mpya ambayo
kwa sasa imejipambanua kutoa huduma za kisasa kulingana na maendeleo ya teknolojia,
mbapo sasa inatoa huduma bora kwa haraka huku ikiwezeshwa na faiba inayotoa
huduma za mawasiliano kwa viwango vya juu.
“nimefurahishwa sana na
jinsi huduma zilivyopanuka kutoka zilivyokuwa maana sasa TTCL inasikika na huduma
zinawafikia watu wengi zaidi,” alisema Malecha.
Akizungumzia suala la
uadilifu Bw. Malecha amesema TTCL ni chombo muhimu kinachotegemewa na Serikali ndio
maana kimeaminiwa na kupewa jukumu la kusimamia miundombinu ya mawasiliano ikiwemo
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) pamoja na Kituo cha Kutunza kumbukumbu
(NIDC).
Amewashauri watendaji wa
shirika hilo kutoiangusha Serikali na hivyo kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa
kuzingatia weledi, uadilifu na uzalendo kwa taifa, huku wakizingatia kuwa chombo
hicho wanachokisimamia ni muhimu sana katika kulinda usalama wa taifa lao.
Alisema ni wazi kuwa teknolojia
ya kuwafikishia wateja huduma yamawasiliano kwa njia ya faiba mpaka majumbani na
ofisini ni huduma inayohitaji watumishi waadilifu na wanaojituma na kulipongeza
shirika hilo kuwa na watu wa aina hiyo ambao wamewezesha huduma hiyo kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wao baadhi
ya wanafunzi walioambatana na Bw. Malecha bandani hapo, wamewaongeza watoa huduma
kwa mapokezi yao na kuweza kuwaeleza shughuli na majukumu ya TTCL kwa wananchi na
Taifa kwa ujumla jambo ambalo limewajenga kiuelewa.
Hata hivyo wananfunzi hao
wamelishauri shirika hilo kuto subiri maonesho ya kitaifa kutoa elimu kwa jamii
bali, kwenda mbali zaidi kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha elimu kuhusu
TTCL inawafikia wananchi wengi zaidi.
“Inaonekana TTCL
inajukumu zito kwa Taifa letu lakini si watu wengi wanalifahamu hilo, na hata hapa
kwenye maonesho wengi wananshindwa kuingia kutokana na kukosa kiingilio hivyo nivizuri
litumie njia mbadala ili kuwafikia watu wengi zaidi,” Alisema Liberatus mmoja wa
wanafunzi hao.
No comments:
Post a Comment