Muonekano wa Barabara ya Kimara – Kibaha (Km
19.2), ambao ujenzi wake kwa njia nane ukiwa unaendelea jijini Dar es Salaam. Muonekano wa Daraja la Mbezi kwa Yusufu katika
Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), ambalo ujenzi wake unaendelea jijini Dar
es Salaam. Muonekano wa Barabara unganishi katika Kituo Kikuu
cha Mabasi yaendayo mikoani cha Mbezi Lous (Stand ya Magufuli) ambayo ujenzi
wake kwa kiwango cha lami unaendelea jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya
akisisitiza jambo kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa Barabara ya Kimara –
Kibaha (Km 19.2), ambao ujenzi wake unaendelea jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya
akisisitiza jambo kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa Barabara ya Kimara –
Kibaha (Km 19.2), ambao ujenzi wake unaendelea jijini Dar es Salaam. Muonekano wa Daraja la Mbezi kwa Yusufu katika
Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), ambalo ujenzi wake unaendelea jijini Dar
es Salaam.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya amemtaka Mkandarasi anayejenga Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), pamoja na Barabara za maingilio katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Mbezi-Magufuli kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Oktoba mwaka huu.
Akizungumza na
wanahabari mara baada ya kukagua barabara hiyo leo jijini Dar es Salaam, Eng.
Kasekenya amesema Serikali imeridhishwa na uboreshaji wa barabara za maingilio
na madaraja katika eneo la mbezi hivyo kumtaka mkandarasi kumaliza kazi hiyo
haraka iwezekanavyo na kwa ubora.
Amebainisha kuwa
katika mkakati wa kupunguza msongamano jijini Dar es salaam tayari maandalizi
ya kujenga kwa njia nane sehemu ya Kimara hadi Ubungo yameanza ili kuhakikisha hakuna
msongamano wa magari kati ya Ubungo-Kibaha.
“..Asilimia themanini na nane iliyofikia
inatosha kukamilisha kazi zilizobaki katika kipindi cha miezi miwili ijayo, hivyo
TANROADS na Mkandarasi ESTIM hakikisheni kazi hiyo inakamilika kwa ubora,”
alisisitiza Eng. Kasekenya.
Aidha amewaonya wezi
wa miundombinu ya taa za barabara kuacha kufanya hivyo mara moja kwani usalama
wa barabara ni pamoja na uwepo wa taa hizo, na kusisitiza umuhimu wa wananchi kutumia
madaraja ya juu na kuvuka katika maeneo yaliyotengwa ili kupunguza ajali.
Naye Mhandisi Mkazi
anayesimamia ujenzi wa Barabara hiyo, Injinia Mwanaisha Rajabu amemhakikishia
Naibu Waziri Kasekenya kuwa atahakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati
na ubora uliokusudiwa ifikapo Oktoba.

No comments:
Post a Comment