BODI YA TTCL YATEMBELEA BANDA LA TTCL MAONESHO YA 46 YA BIASHARA DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 4 July 2022

BODI YA TTCL YATEMBELEA BANDA LA TTCL MAONESHO YA 46 YA BIASHARA DAR


Kaimu  Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bw. Richard Mayongela (mwenye suti ya blue) akipewa Maelezo ya vifaa vya Mawasiliano kutoka kwa watumishi Shirika hilo alipotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula akibadilishana mawazo na Viongozi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania alipotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya watumishi Shirika la Mawasiliano Tanzania wakiwahudumia wateja waliofika katika Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Wateja wakiendelea kupatiwa huduma katika Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya T-Pesa Dkt. Muba Seif (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bw. Richard Mayongela ( wa pili kushoto) wakipata Maelezo kutoka kwa Mkutugenzi wa Biashara wa TTCL kuhusu huduma ya Faiba Mlangoni Kwako wakati walipotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Biashara Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)Bw. Vedastus Mwita (kuliamwenye suti) akimfafanua jambo kuhusu huduma ya Faiba Mlangoni Kwako,kwa  Kaimu  Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bw. Richard Mayongela (wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya T-Pesa Dkt. Muba Seif (wa pili kushoto) walipotembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya 46 ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) Dar es Salaam.

Tupo tayari kuwahudumia wateja Sabasaba; Maafisa kutoka Shirika la Mawasiliano wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa kuwahudumia wateja wanaofika katika Viwanja vya Sabasaba kwa ajili ya maonesho ya 46 ya Biashara.

Mkurugezi Mkuu Shirika la Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga akimsikiliza kwa makini Afisa Mwandamizi Idara ya Uzalishaji Bidhaa na Utafiti wa Masoko Bw. John Yahaya alipokuwa akimwelezea moja ya miundombinu ya Mawasiliano ya Mkongo wa Taifa mbayo ni Metroduct kwa ajili ya kupitisha Faiba ili kuwezesha huduma za Mawasiliano kwa mtumiaji wa mwisho.

No comments:

Post a Comment