NMB YASHIRIKI NA KUDHAMINI WIKI YA UBUNIFU DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 18 May 2022

NMB YASHIRIKI NA KUDHAMINI WIKI YA UBUNIFU DODOMA

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi akizungumza na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, alipotembelea Banda la NMB wakati wa maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Maafisa wa NMB katika picha ya pamoja wakiwa kwenye banda lao, wakati wa maonesho ya Wiki ya Ubunifu yanayoendelea jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi  na Teknolojia -  Prof. Adolf Mkenda ameishukuru Benki ya NMB kwa kushiriki na kudhamini maonesho  ya Kitaifa ya Wiki ya Ubunifu, yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolijia, kuanzia tarehe 20 Mei  katika uwanja wa Jamhuri - jijini Dodoma.

Aidha, Profesa Mkenda aliongeza kuwa, benki hiyo imekuwa karibu na Wizara hiyo hata katika utoaji wa mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya Diploma mpaka Shahada, hivyo kusaidia wanafunzi wengi kujiunga na vyuo kuanzia mwaka ujao wa masomo. 

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi alimueleza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman alipotembelea Banda la NMB kuwa, NMB inathamini  ubunifu na imekuwa ikiibuka na masuluhisho bora ambayo yamekuwa na manufaa kwa Benki na Sekta ya Fedha kwa ujumla.

"Tunathamini sana ubunifu kwani kwa kupitia hiyo, tumewaletea wateja wetu na watanzania kwa ujumla masuluhisho kama Mshiko Fasta, Lipa Mkononi na NMB Pesa Wakala ambazo zinapunguza wingi wa wateja kufika matawini kupata huduma," alisema Mlozi 

Lakini pia, Nsolo alisema NMB imeandaa fursa maalum kwa wabunifu mbalimbali hususani wa masuluhisho ya kifedha kujaribu suluhishi zao za kiteknolojia kabla ya kuziingiza sokoni.

No comments:

Post a Comment