RAIS SAMIA HASSAN AZINDUA NA KUGAWA VITENDEA KAZI KWA MAAFISA UGANI KILIMO NCHINI JIJINI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 4 April 2022

RAIS SAMIA HASSAN AZINDUA NA KUGAWA VITENDEA KAZI KWA MAAFISA UGANI KILIMO NCHINI JIJINI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akielezea kuhusu vitendea kazi kwa Maafisa Ugani Kilimo kabla ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda la NMB kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa Ugani Kilimo Nchini uliofanyika jana Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu zao la parachichi ambalo limekuwa likiwaletea tija wakulima nchini hususan katika Mikoa ya Njombe, Mbeya, Arusha na Kilimanjaro.

Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi na ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04, Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.


No comments:

Post a Comment