MKE WA MAKAMU WA RAIS MAMA MPANGO AZINDUWA LOGO MPYA YA IIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 25 March 2022

MKE WA MAKAMU WA RAIS MAMA MPANGO AZINDUWA LOGO MPYA YA IIA

Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa logo mpya ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), CPA Zelia Njeza, pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia.

 

Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua logo mpya ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) leo jijini Dar es Salaam. 

Na Mwandishi Wetu

MKE wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango, amesema wakaguzi wa mahesabu ya ndani wakitumika vizuri wanaweza kuchochea zaidi maendeleo ya taifa. Uwepo wa wakaguzi wa ndani wa mahesabu ndani ya Serikali, mashirika, taasisi za umma na binafsi unasaidia taasisi hizo kufuata taratibu na kanuni za kimatumizi hali ambayo usaidia kufanya vizuri zaidi na kuchochea maendeleo.

Mama Mpango ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa logo mpya ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) pamoja na tovuti ya taasisi hiyo ili kwendana na mabadiliko yanayoendelea.

Alizitaka taasisi zinazokaguliwa na kupewa ushauri na wakaguzi hao kutoa ushirikiano na kufanyia kazi ushauri wanaopewa, kwani maendeleo hayawezi kupatikana kama kutakuwa na matumizi yasiyozingatia sheria, kanuni na miongozo ya matumizi.

"Wakaguzi wa ndani wanamchango mkubwa katika maendeleo sehemu yoyote, iwe kwenye ofisi za Serikali, taasisi za umma na hata zile za binafsi. Sehemu yoyote kama hakuna usimamizi mzuri wa matumizi maendeleo hayawezi kupatikana," alisema Mama Mpango.

Kwa upande wake Rais wa IIA-Tanzania, CPA Zelia Njeza akizungumza awali katika hafla hiyo, alisema taasisi hiyo imefanya utafiti kwa muda mrefu na kubaini kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ya logo yake ili kuendana na mabadiliko ya sasa. 

"Tumefanya utafiti wa muda mrefu kabla ya kufikia hatua hii, na kubaini upo umuhimu wa kufanya mabadiliko kwendana na maendeleo na mabadiliko ya sasa," alisema CPA Njeza akizungumza.


Rais wa IIA-Tanzania, CPA Zelia Njeza akizungumza akifafanua kwa wadau juu ya logo mpya ya IIA. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Fatma Khamis Mohamed.


Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), CPA Zelia Njeza akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa logo mpya ya IIA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Fatma Khamis Mohamed akizungumza na wanahabari kwenye hafla ya uzinduzi wa logo mpya ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA) leo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), CPA Zelia Njeza akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa logo mpya ya IIA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 


Sehemu ya wadau wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani nchini Tanzania (IIA), wakifuatilia hafla hiyo.



No comments:

Post a Comment