WASHINDI 100 WA NMB MASTABATA WANYAKUA 10M/- - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 6 January 2022

WASHINDI 100 WA NMB MASTABATA WANYAKUA 10M/-

Meneja Mwandamizi wa wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kampeni ya MastaBata Kivyakovyako iliyochezeshwa Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi, Manfred Kayala, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya.

Meneja Mwandamizi wa wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite akichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya MastaBata Kivyakovyako iliyofanyika, Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi, Manfred Kayala, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya na kulia ni Doleen Masonda wa Idara ya Kadi wa Benki ya NMB.

Meneja Mwandamizi wa wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite akichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya MastaBata Kivyakovyako iliyofanyika, Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi, Manfred Kayala, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya na kulia ni Doleen Masonda wa Idara ya Kadi wa Benki ya NMB.

PROMOSHENI ya MastaBata-Kivyako Vyako ilizinduliwa rasmi katikati ya mwezi Disemba mwaka jana kwa lengola kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za Mastercardkama sehemu ya mchango wa NMB katika juhudi zataifa za kujenga uchumi usiotegemea sana fedhataslimu.

NMB pia inatumia kampeni hii ya kuendeleza uchumi wakidijitali kurudisha fadhila kwa wateja wake waaminifuambao wamekuwa ni muhili muhimu wa safari yake yamabadiliko ya kidijitali.

Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata washindi wakwanza wa MastaBata-Kivyako Vyako, Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ally Ngingite, alisema zaidi ya TZS milioni 200 zitanyakuliwakwenye kampeni hii ya miezi mitatu.

“Hili ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanzarasmi mwaka 2018 kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za Mastercardwanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti,” mtaalumu huyo wa mikopo binafsi alisema.

“Kama watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo la kuwatambua nakuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendeleakutumia huduma zetu,” Bw Ngingite aliongeza nakutabainisha kuwa zitakuwepo pia droo za kila mwezi naile kubwa ya mwisho.

Wakati washindi 100 wa kila wiki watashinda TZS 100,000 kila mmoja, 25 watanyakua TZS 1,000,000 kilamwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya TZS milioni 90 zikiwa ni TZS milioni kwa kila mshindi.

Bw Ngingite alisema takribani wateja 1,000 wanategemewa kushinda zawadi za promosheni yaMastaBata-Kivyako Vyako iliyopangwa kufikia tamatimwezi Machi.

Kampeni hii inawahusisha pia wateja wa benki hiyowanaofanya malipo kwa NMB MasterPass QR. Kama kawaida droo ya jana ilisimamiwa na ofisa mwandamiziwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

NMB inasema kampeni zake za MastaBatazimefanikiwa sana kuchagiza malipo ya kidijitali nchinina matumizi ya kadi za Mastercard kufanya malipo namiamala mbali mbali.

Mwezi Novemba mwaka jana, kampuni ya Mastercard International iliitunuku NMB tuzo maalumu ya kuwabengi kiongozi wa kuhamasisha matumizi ya kadi zakenchini.


No comments:

Post a Comment