SPIKA NDUGAI AACHIA NGAZI, MAJI YAMFIKA SHINGONI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 6 January 2022

SPIKA NDUGAI AACHIA NGAZI, MAJI YAMFIKA SHINGONI...!

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametangaza kujiuzulu wadhifa wake leo Januari 6, 2022 kutokana na mvutano uliotokea kufuatia kauli yake aliyoitoa akimshutumu Rais Samia Suluhu kukopa Tsh trilioni 1.3.

Kwa mujibu wa barua yake ya kujiuzulu ambayo Ndugai ameiwasilisha kwa Karibu Mkuu wa CCM na nakala kwa Karibu wa Bungee, amesema amechukua hatua hiyo kwa hiari na kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa, serikali na CCM.

Aidha Ndugai ametoa shukrani za dhati kwa Wabunge, Rais Samia Suluhu Hassan wananchi wa jimbo la Kongwa na watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment