Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Mjini Mussa Sima amefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya barabara na maeneo korofi ili yatafutiwe ufumbuzi.
Akizungumza katika ziara hiyo aliyoifanya leo alisema anataka kuona maeneo yote korofi katika barabara zote ziliopo jimboni humo yanatafutiwa ufumbuzi kwa kuyamaliza haraka iwezekanavyo.
"Hakuna sababu ya kuwa na maeneo korofi kwenye barabara zetu wakati Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ametupa Sh. 2.2 Bilioni kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara nachukua nafasi hii kumpongeza kwa niaba ya wananchi wa jimbo letu" alisema Sima.
Maeneo aliyoyatembelea ni barabara inayotengenezwa Mwamise na Unyankhae Kata ya Mandewa pamoja na kuangalia maeneo korofi yanayohitaji kufanyiwa kazi yaliyopo Mtaa wa Mnung’una Kata ya Minga.
No comments:
Post a Comment