Gari iliopata ajali na wanahabari hao. |
WAANDISHI watano wamefariki dunia kwa ajali ya gari walipokuwa katika msafara wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Taarifa zinasema ajali hiyo ilitokea baada ya gari la Serikali lililowabeba wanahabari hao kugonga na Hiace eneo la Busega likiwa safarini kuelekea Ukerewe kupitia Bunda.
Walio fariki katika ajali hiyo ni HUSNA MLANZI- ITV, JOHARI SHANI - Uhuru Digital, ABEL NGAPEMBA- AFISA HABARI MKOA wa Mwanza, ANTHONY CHUWA -HABARI LEO DIGITAL pamoja na STEVEN MSENGI- AFISA HABARI wa UKEREWE.
Taarifa zaidi zinasema katika ajali hiyo watu wengine 9 waliokuwa kwenye Hiace wamefariki pia. Taarifa zaidi tutawaleteeni baadaye. Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu hao.
Taarifa ya Mwanza Press Club inaeleza:
"Tunasikitika kutangaza vifo vya Wanatasnia wenzetu watano kilichotokea leo asubuhi kwa ajali ya gari iliyohusisha gari la Serikali na Hiace.
Waliopoteza maisha kwa taarifa kutoka Mwanza Press Club:
1. HUSNA MLANZI- ITV
2. JOHARI SHANI - Uhuru Digital
3. ABEL NGAPEMBA- AFISA HABARI MKOA
4. ANTHONY CHUWA -HABARI LEO DIGITAL
5. STEVEN MSENGI- AFISA HABARI UKEREWE
No comments:
Post a Comment