KAMPENI ya Benki ya NMB ya kuwahamasisha wateja wake kuweka akiba ya Bonge la Mpango II ilifungwa rasmi wiki iliyopita kwa washindi 32 kujinyakulia zawadi zenye thamani ya TZS milioni 100.
Miongoni mwa washindi wa droo ya mwisho ya promosheni hiyo kabambe walikuwa ni wateja 22 wa NMB walioshinda pikipiki za miguu mitatu aina ya Skymark ambazo bei ya kila moja ni TZS Milioni 4.5.
Pia katika kuhitimisha shindano hilo la wiki 12 lililoanza mwezi Oktoba mwaka jana washindi 10 walishinda TZS 100,000 kila mmoja. Lengo la “Bonge la Mpango II” ilikuwa kurejesha fadhila kwa wateja waaminifu na kuwahamasisha kujenga utamaduni wa kuweka akiba, na promosheni hii imenufaisha wateja zaidi ya 170.
Kwenye droo ya mwisho iliyofanyika katika Tawi la NMB Bagamoyo mbele ya Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bi Pendo Mfuru, washindi 17 walitwaa pikipiki za fainali, watatu wakijibebea pikipiki za mwisho wa mwezi na wawili walishinda pikipiki za droo ya wiki.
Hii imekuwa promosheni yenye mafaniko makubwa sana, kwani kila wiki washindi 10 walijishindia pesa taslimu na wawili pikipiki za Skymark, huku droo za mwisho wa mwezi zikiwazawadia washindi watatu pikipiki hizo za kisasa. Jumla ya Skymark 50 zilinyakuliwa kwenye kampeni hii iliyokuwa na zawadi zenye thamani ya zaidi ya TZS. Milioni 246 ambazo washindi wake walitoka sehemu mbalimbali nchini.
Washindi walioshinda pikipiki za droo ya mwezi Desemba na matawi yao kwenye mabano ni: Emmanuel Kavishe (Zanzibar), Mbila Salum (Mafinga) na Albert Mhehe (Mkwawa).
Waliojinyakulia pikipiki 17 za droo ya fainali ni: Frank Mgeni (Ngaramtoni), Bundala Gwanona (Geita), Mary Martine (Kenyatta Road), Misoji Joseph (Kenyatta Road), Martha Makorere (Tarime), Ambakisye Kyomo(Kaitaba), Paschal Kaloli (Geita) na Herieth Alphonce (Babati).
Wengine ni Elineema Ezekiel (Babati), Khamis Abbas (Sikonge), Hamalos Kahindi (Nzega), Mathias Lusendamila (Manonga), Clement William (Wami), Michael Kabume (Mvomero), Glory Mwalongo (Mvomero), Marc Constantine (Wami) na Aziza Nzoto (Mvomero).
No comments:
Post a Comment