Wasumbwa. |
Na Adeladius Makwega, Dodoma
KATIKA matini yangu iliyotangulia juu ya Kabila la Wasumbwa msomaji wangu unakumbuka nilivyokusimulia utani baina ya Wasumbwa, Wazaramo na Wagogo na namna Wagogo walivyoshiriki kuuvamia msafara ya Chifu wa Wasumbwa Kafuku na kumuua na hata mwisho nilimalizia madhara yaliyowapata Wagogo hadi walipofunga safari hadi Kahama kwa ndugu wa Chifu Kafuku kuwaomba msamaha kwa tukio hilo.
Unakumbuka msomaji wangu pia nilisimulia namna Wagogo walivyotakiwa kutoa fidia ya mifugo 300 na hapo ndipo msamaha ulikubaliwa na ndugu wa Chifu Kafuko kufika Dodoma na kuichukua pembe iliyokuwa ikisababisha ukame na njaa katika makaazi ya Wagogo na kuichoma moto.
Kwa msomaji wangu, naomba ukumbuke kuwa Wasumbwa kama walivyoelewana sana na Wazaramo kwa kuwafafanisha na Wanyamwezi kumekuwa na hoja moja kubwa mbili, Lugha ya Kisumbwa inalingana kwa karibu na Kinyamwezi na pia Wasumbwa kuna wakati waliaminika walikuwa chini ya Chifu Mirambo. Ndani ya hilo kuna hoja kuwa na hata maandiko machache mno yaliyoandikwa juu ya kabila hili na machifu wake, kw ahiyo halifahamiki sana.
Wazaramo waliwatazama Wasumbwa kama Wanyamwezi kwa kuwa walikuwa wakitokea eneo ambalo ndilo Wanyamwezi wakitokea .”Twekupuna eyo kupunila mwezi.” Ikimaanisha kuwa tunatokea huko unakotokea mwezi (Wanyamwezi)-Those who produce moon.
Wasumbwa wana kitu tofauti na makabila mengine hasa suala la mahusiano baina ya binamu wa kike na wakiume, hawa huwa ni ndugu kabisa yaani kaka na dada na hakuna mahusiano ya kimapenzi wala kuoana baina yao. Hawa wanaheshimiana kabisa kama kaka na dada wanaozaliwa tumbo moja, ndiyo kusema mtoto wa mjomba na shanganzi hawawezi kuoana.
Wasumbwa wana utani kama nilivyokujulisha na Wazaramo, Wagogo, Wanyamwezi na na pia na Wangoni, pale mtani wao anapofariki hali ya utani huwa mara dufu kwa kusema kuwa “Tukulya mno bwalelo.” Kwamba leo tutakula mno, kwa kuwa mtani amefariki, hali hii ya utani inaweza pia kuwapo kati ya koo na koo za Kisumbwa zenyewe.
Wasumbwa kama yalivyo makabila mengine na wao ni mabingwa wa kutambika na ya siku ya kutambika huwa wanaandaa pombe ya tambiko ambapo kwa wale watani siku ya tambiko hilo uibuka na kuichukua pombe ya tambiko na kuinywa bila ya kuogopa madhara yoyote yatakayotokea kwao kwani pombe ya tambiako huwa inaheshimika sana kwa ajili ya mizimwi. Mtani anaweza kufika wakati wa tambiko akaichukua na kuinywa huku akisema kuwa “Misamba yilabafile hi?.” Hivi nyie haya matambiko mnadhani yatawafikisha wapi?
Hapo juu nilikujulisha kuwa kabila lingine lenye utani na Wasumbwa ni Wangoni, kama ilivyo desturi Wangoni walikuwa mabingwa wa vita na ukitazama makabila mengi yana utani na Wangoni, kwa hiyo hilo limefanya hata Wasumbwa kuwa na utani na ndugu hawa ikiaminika kuwa Wagoni walipokuwa wakipigana waliwahi kufika eneo la Busumbwa na hapo ndipo utani ukaanza. Wasumbwa kwa Wangoni wanatazamwa kama“Bafu bakadeni.” Ikimaanisha watu wa kuuwawa tu. Mtu wa namna hiyo ni sawa na mtumwa. Utani huo na kivita ulisabisha kukawepo na urafiki mkubwa wa Wasumbwa na Wangoni.
0717649257
No comments:
Post a Comment