HALMASHAURI ya Wilaya ya Nyasa imetoa mkopo wa pikipiki 5, na fedha Taslim Sh Milioni 37 kwa ujumla, kwa Vikundi vya wajasiliamali vya Wanawake walemavu na Vijana.
Hafla ya kuwakabidhi wanakikundi hao imefanyika hivi karibuni, katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa, na Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas.
Akikabidhi Mikopo hiyo kwa wanakikundi, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kanali Laban Thomas ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, kwa kutoa mikopo hiyo kwa wajasiliamali ikiwa ni Fedha za asilimia kumi ya mapato ya Ndani, ambayo hukusanya Halmashuri na kuyapa makundi hayo maalum kwa lengo la kuongeza kipato kwa jamii.
Ameongeza kuwa Halmashauri imepiga hatua kubwa ya Kumkopesha Mlemavu mmoja pesa Taslim,Pikipiki 5 kwa kikundi cha Vijana na Wanawake wakipewa mkopo wa fedha Taslim.
Ametoa mchanganuo wa ugawaji wa mikopo kwa wanawake wamekopeshwa tsh 14,800,000 vijana Pikipiki 5 zenye thamani ya Tsh Milioni 13,500,000 na walemavu 8,7000,000.
Aidha ametoa wito kwa wanavikundi hao kuthamini mchango wa Halmashauri, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ,hivyo wanatakiwa kurudisha fedha hizo kama mikataba yao inavyosema, ili fedha hizo zikirudishwa kwa wakati ili waweze kupewa wanakikundi wengine kwa lengo la kupanua wigo na kujilea maendeleo.
“Rai yangu kwenu ni kuhakikisha kuwa wote waliopewa fedha wanatakiwa kurudisha kama mikataba yao inavyosema, ili na wengine nao wawe wanapewa mikopo hiyo”.
Awali akitoa Taarifa fupi Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya nyasa, Ndugu Jimson Mhagama amesema Halmashauri ya Nyasa kwa sasa imejiwekea malengo ya kutoa mikopo ya vitu, Badala ya Fedha Taslimu ambazo haziwanufaishi walengwa kwa kuwa wanagawana kidogo kidogo na hawafikii malengo waliyojiwekea, lakini kama watapatiwa mikopo ya Vitu Kama Pikipiki, au mashine ya kusaga ili yaweze kutoa huduma na kuajiri wanakikundi wengine kama kuchakata unga na kazi zingine watafanikiwa zaidi.
Akifafanua Kuhusu utoaji Mikopo amesema tangu Halmashauri ianze haijawahi kutoa mikopo ya Vitu kama Bodaboda na Mlemavu Mmoja, kwa hiyo leo ni siku ya Kihistoria Wilayani hapa na tunashuhudia Halmashauri ikiwainua kiuchumi makundi maalum ya Vijana, Watoto, na Wanawake.
Amezitaja Kata zilizonufaika ni Liwundi, Lituhi, Mbaha, Liuli, na Kilosa. Na kwa upande wao wanakikundi wanufaika wa mikopo hiyo wamesema wanaipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwapa mikopo hiyo na wameahidi kuitumia vizuri ili kuongeza ukuaji wa biashara zao.
No comments:
Post a Comment