Na Lorietha Laurence-Arusha
NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Kipanga Juma Omary ameipongeza kamati ya mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa hatua nzuri ya awali ya ujenzi wa mradi huo .
Mhe.Kipanga ameyasema hayo Januari 29,2022 Jijini Arusha wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo unatakaogharimu kiasi cha Shilingi Bilion 16.7 wenye uwezo kuchukua wanafunzi wasiopungua 500 pamoja na vyumba 42 kwa ajili ya akina mama wenye watoto wadogo na mahitaji maalum.
“kazi iendane na muda ulipopangwa , kwa sasa mkandarasi upo nyuma ya muda hivyo jitahidi kuhakikisha unaratibu na kusimamia vizuri watenda kazi wako ili kufanikisha na kuweza kukabidhi mradi ifikapo Oktoba, 2022”anasema Mhe.Kipanga
Aidha Mhe. Kipanga amemtaka Makandarasi kuzingatia rasilamlia tano za ujenzi ambazo ni fedha, vifaa, kazi, muda na usimamizi ili kutekeleza mradi kwa muda uliopangwa.
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Emmanuel Luoga ameahidi kushirikiana kwa karibu na wataalam kutoka Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na kuzingatia ubora.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Dr.Kelvin Mtei amemshukuru Naibu Waziri Mhe. Kipanga kwa mawazo aliyoyatoa wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi na kuahidi kufanyia kazi maboresho yote aliyoyatoa.
Mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi unatarajiwa kutekelezwa kwa awamu tatu ambapo awamu inayotekelezwa sasa ni ya kwanza inagharimu shilingi bilioni 1.6 fedha kutoka Vituo vya Umahiri vya Benki ya Dunia CREATES na WISE FUTURES ambao umeanza Oktoba 2021 na unatarajiwa kukamilika Oktoba 2022 ,ikiwa ni jengo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 180 vikiwemo vyumba 24 vya akina mama wenye watoto wadogo.
No comments:
Post a Comment