SERIKALI IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA - DKT. HASHIL ABDALAH - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 3 December 2021

SERIKALI IMEJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA - DKT. HASHIL ABDALAH

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa   Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India, Disemba 2, 2021, Diamond Jubilee, Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akikagua Bajaji wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India, Disemba 2, 2021, Diamond Jubilee, Dar es salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah kuangalia koponi ya mshindi wa bahati na sibu iliyoendeshwa wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India, Disemba 2, 2021, Diamond Jubilee, Dar es salaam.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akioneshwa moja ya gari mara baada ya kuzinduwa Maonyesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka India.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (wa pili kulia) akiendelea kutembelea maonesho ya Bidhaa za Usafirishaji kutoka nchini India.

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil  Abdalah amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuimarisha sekta ya viwanda na biashara kwa kuhakikisha wafanyabiashara wananufaika na Serikali inanufaika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya bidhaa za usafirishaji ambazo zinaingizwa nchini kutoka  India katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Disemba 2, 2021 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari, wafanyabiashara na wananchi waliofika katika maonyesho hayo Dr. Abdallah amesema Maonyesho hayo ni muhimu katika kukiza uchumi wa nchi  kwa kuwa vifaa vya usafirishaji kama Pikipiki, Bajaji, Matrekta magari vinatumiwa na wananchi wengi katika kurahisisha shughuri zao za kila siku.

"Bidhaa hizi mfano Matrekta, Bajaji, Pikipiki zinaingia sokoni kama mitaji ambayo inatumika na watu kujiendeleza kiuchumi," Amesema  Dkt. Absallah.

Aidha, Dkt. Abdallah amesema Wizara ya Viwanda na Biashara ipo tayari kutoa  ushirikiano na kutatua changamoto ambazo zinawakabili wafanya biasharawakati wowote  kwa kushirikiana na wadau wengine. 

Naye,  Balozi wa India  nchini Tanzania, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema ingawa kwa sasa bidhaa hizi zinazalishwa nchini India, hivi karibuni zitaanza kuzalishwa nchini Tanzania.

Dkt. Abdallah ametoa rai kwa watanzania kufika katika maonyesho hayo kuzungumza moja kwa moja na wafanyabiashara na benki zilizopo hapo ili kuona namna ya kutumia fursa hii kujinufaisha.

No comments:

Post a Comment