BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA “TISHA NA TEMBOCARD VISA,” WATEJA 4 KUPELEKWA KUSHUHUDIA AFCON 2022 NCHINI CAMEROON - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 2 December 2021

BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA “TISHA NA TEMBOCARD VISA,” WATEJA 4 KUPELEKWA KUSHUHUDIA AFCON 2022 NCHINI CAMEROON

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akionyesha aina mpya ya kadi za ‘TemboCard’ wakati wa hafla ya uzindunzi wa kampeni ya Tisha na TemboCardVisa ulioenda sambamba na uzinduzi wa kadi hizo uliofanyika leo katika Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mkuu wa Idara wa Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda (Kulia) na Kaimu Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi wa Benki hiyo, Erica Mwaipopo.
 

Benki ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya Visa international leo imezindua kampeni ya “Tisha na TemboCard Visa” inayolenga kuhamasisha wateja kujenga utamaduni wa kutumia kadi zao za TemboCardVisa huku wakijiwekea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo kushuhudia kombe la mataifa ya afrika AFCON litakalofanyika nchini Cameroon mwakani 2022.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Wateja wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Rabala alisema zawadi zitatolewa kwa wateja ambao watafanya miamala mingi zaidi kupitia TemboCardVisa zao katika kipindi chote cha kampeni ambayo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Machi 2022.

“Lengo letu ni kuona wateja na Watanzania wanajenga utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo ya manunuzi na kuachana na utaratibu wa kutumia pesa taslimu ambazo sio salama. Katika kipindi hiki cha kampeni tutatoa zawadi kwa washindi zaidi ya 80 ambapo kila mwezi tutao zawadi kwa washindi 20,” alisema Raballa.

Akielezea kuhusu zawadi zitakazotolewa katika kampeni hiyo, Raballa alisema wateja watapata zawadi mbalimbali ikiwamo kurudishiwa asilimia 5 ya kiasi walichotumia, kulipiwa bili ya malipo ya manunuzi, simu janja, tablet, televisheni, sofa set, home theatre, pamoja na safari ya kitalii kwenda Zanzibar au Serengeti. “Kubwa zaidi ni zawadi ya safari ya kwenda Cameroon kushuhudia michuano ya AFCON kwa wateja 4 ambao watakuwa na miamala mingi zaidi katika kipindi cha Desemba na Januari. Washindi wataruhusiswa kwenda na wenza au rafiki zao” alisema Rabala.

Raballa alitoa rai kwa wateja wa Benki hiyo na Watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo kwa kutumia kadi zao za TemboCardVisa kufanya malipo huku akiwasihi kuendelea na utamaduni huo hata baada ya kampeni kwani lengo ni kufanya matumizi ya kadi kuwa sehemu ya kawaida ya miamala ya malipo ikiwa ni mkakati wa kujenga jamii yenye matumizi machache ya pesa taslimu “cashless society”.

“Kwa wale ambao hawana akaunti niwashauri wafungue akaunti ili waweze kuunganishwa na TemboCardVisa na kuanza kufurahia huduma huku wakijiwekea nafasi ya kujishindia zawadi kemkem. Kama mnavyojua sasa hivi zoezi la kufungua akaunti tumelirahisisha sana…”

“…kama una simu janja unachotakiwa kufanya ni kupakua SimBanking App na kufuata hatua za kufungua akaunti kwa kutumia namba ya NIDA na kisha utaomba kupata TemboCard yako, kwa wale wa sio na simu janja wanaweza kutembelea kwa CRDB Wakala wakiwa na kitambulisho cha NIDA kufunguliwa akaunti na kupata TemboCardVisa kwa urahisi. Tunatamani kuona watu wengi zaidi wakishiriki ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo,” aliongezea.

Awali akielezea namna ya kushiriki katika kampeni hiyo na kuibuka mshindi, Kaimu Meneja Mwandamizi wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Erica Mwaipopo alisema wateja wanatakiwa kutumia kadi zao za TemboCardVisa kulipia manunuzi na huduma katika maduka, supermarkets, migahawa, hoteli na vituo vya mafuta kupitia vifaa vya manunuzi (POS), pamoja na malipo ya mitandaoni ikiwamo kulipia tiketi za ndege au malipo ya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

Uzinduzi huo wa kampeni hiyo ya “Tisha na TemboCardVisa” ulienda sambamba na uzinduzi na muonekano mpya wa kadi za Benki ya CRDB ‘TemboCard’ ambazo zimeboreshwa zaidi ili kuwapa wateja uzoefu bora zaidi pindi watumiapo kadi zao. Akielezea kuhusu ujio wa kadi hizo mpya za TemboCardVisa, Mkuu wa kitengo cha Masoko, Joseline Kamuhanda alisema kadi hizo zimetengenzwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayowawezesha wateja kutumia kadi zao kwa urahisi kufanya malipo popote pale.

Benki ya CRDB ilikuwa benki ya kwanza kuanzisha huduma za kadi ‘TemboCard’ nchini mwaka 2002, ikilenga kuwapa wateja wake urahisi na unafuu wa upatikanaji wa huduma popote walipo. Mpaka sasa Benki ya CRDB imefanikiwa kutoa zaidi ya TemboCard milioni 3 ikiungana na mifumo ya malipo ya kimataifa ya Visa, MasterCard na Union Pay.  Huduma za Tembocard zimechangia kwa kiasi kikubwa kusaidia jitihada za serikali katika kuimarisha mfumo wa malipo nchini na kuongeza ujumuishi wa kifedha “Financial Inclusion”.






No comments:

Post a Comment