TANZANIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MCHEZO WA SOKA KWA WENYE ULEMAVU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 2 December 2021

TANZANIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA MCHEZO WA SOKA KWA WENYE ULEMAVU

 

Wachezaji wa Tembo Warriors wakishangilia baada  ya mechi kuisha.

Viongozi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa  na katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi wakishangilia  ushindi wa timu ya Tembo Warrior kufuzu kuingia Kombe la Dunia  Oktoba 2022 nchini Uturuki.

Wachezaji wa Tembo Warriors wakishangilia  kwa  mtindo wa aina yake mara baada ya  kufunga  goli  la kwanza.

Na John Mapepele

 

WAZIRI mwenye dhamana ya Michezo nchini. Mhe, Innocent Bashungwa leo Disemba 1, 2021 amewaongoza watanzania kuishangilia Timu ya Tanzania (Tembo Warriors) ambayo imefuzu na kuwa  timu ya kwanza miongoni mwa timu nne zinazoingia nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa   wenye ulemavu (CANAF 2021) na hivyo kupata tiketi ya kushiriki  Mashindano ya Dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon  mabao 5-0. 

 

Timu ya TTtanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na  Kamati Maalum ya Kitaifa  chini ya Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassani Abbasi ilianza vizuri  kutokana hamasa  iliyotolewa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hasan.

 

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo Tembo ilishinda goli 1-0.

 

 Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hii, Mhe. Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri maandalizi ya Kombe la Dunia.

 

 Aidha, Dkt Abbasi amesema kwa kuwa safari ya kuelekea kombe la dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa kombe linabaki Tanzania.

 

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15, Ramadhan Chomole  dakika ya  18, na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

 

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa Mashindano hayo duniani Mateus Wildack.

No comments:

Post a Comment