ZAIDI YA BILIONI 12 ZIMETOLEWA KUKAMILISHA MIRADI YA BARABARA VIJIJINI SINGIDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 2 December 2021

ZAIDI YA BILIONI 12 ZIMETOLEWA KUKAMILISHA MIRADI YA BARABARA VIJIJINI SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kulia) akikata utepe kuzindua hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi na matengenezo ya Barabara kati ya Wakandarasi na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani singida leo Tarehe 1 Desemba 2021. Wengine katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma Kilimba na Mratibu wa Tarura Mkoa wa Singida, Mhandisi Tembo Davascar.

Dkt Mahenge akionyesha mwonekano wa mkataba huo.

Dkt Mahenge akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma Kilimba akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mratibu wa Tarura Mkoa wa Singida, Mhandisi Tembo Davascar akitoa taarifa fupi ya mwenendo mzima wa zoezi hilo.

Wahandisi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.

Wahandisi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.

Zoezi la Utiaji saini wa mikataba hiyo likiendelea.

Godwin Myovela, Singida

ZAIDI ya shilingi 12 bilioni zimetolewa na serikali kwa idadi ya kandarasi 26 kwa ajili ya matengenezo ya barabara za vijijini mkoani hapa.

Mpaka sasa mikataba 26 ya matengenezo ya barabara hizo yenye thamani ya shilingi bilioni 12.6 tayari imesainiwa kati ya Wakandarasi na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini mkoani hapa (TARURA) huku Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, mkoa wa Singida  Alhaji Juma Kilimba wakishuhudia zoezi hilo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa Tarura mkoa wa Singida, Mhandisi Tembo Davascar, alisema mikataba hiyo 26 ya awamu ya pili itahusisha matengenezo na ujenzi wa barabara zilizopo wilaya za Ikungi, Manyoni, Mkalama, Itigi, Iramba na Singida Vijijni.

Hata hivyo, Davascar alisema wametoa siku 14 kuanzia sasa kwa wazabuni hao kujipanga na kuandaa vikosi kazi vyao na baada ya hapo watatakiwa kutekeleza mikataba yao ndani ya kipindi kisichozidi miezi 6 baada ya siku hizo

“Ratiba ya utekelezaji wa hii mikataba itaanza siku 14 kuanzia sasa, na kuanzia Desemba 15 wanapaswa kuanza mara moja utekelezaji wa mkataba kwa kipindi kisichopungua miezi 6,” alisema.

Awali akizungumza kabla ya zoezi la utiaji saini, Dkt Mahenge aliwahimiza na kuwakumbusha wakandarasi kuzingatia kikamilifu ratiba ya utekelezaji wa mikataba hiyo bila ya kuingiza visingizio vyovyote vinavyoweza kukwamisha ustawi wa miradi hiyo muhimu kwa maendeleo

Aidha, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia ubora na viwango sambamba na kutanguliza uzalendo wakati wa utekelezaji wake kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa ambazo ni chimbuko la kodi za wananchi katika muktadha chanya wa matumizi endelevu kwa vizazi vya sasa na baadaye.

“Nikiwatazama wahandisi wote hapa mnaosaini mikataba ya ujenzi wa barabara hizi ni wazawa, sitarajii kuona virusi vyovyote vinajitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hii ambayo Mheshimiwa Rais ameamua bilioni hizi 12.6 zielekezwe kwetu kwa ajili ya barabara za vijijini pekee…naomba tusimwangushe, na tusiwaangushe walipa kodi waliowezesha hili kufanyika,” alisema Dkt. Mahenge

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akiwa miongoni mwa walioshuhudia zoezi la utiaji saini alipongeza serikali kupitia chama hicho kwa kutekeleza yale yalioelekezwa kwenye ilani

No comments:

Post a Comment