MHE. RAIS SAMIA AZINDUA MWONGOZO WA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE NA KUPOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS MUSEVEN - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 28 October 2021

MHE. RAIS SAMIA AZINDUA MWONGOZO WA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE NA KUPOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS MUSEVEN

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addou, Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante O. Gabriel.


Hafla ya uzinduzi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi mkazi wa UN Women hapa nchini bibi.  Hodan Addou, kulia Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 28 Oktoba 2021 ameshiriki katika mjadala kuhusu Kipindi cha mpito wa haki wa tabianchi ulioendeshwa kwa njia ya mtandao na Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni, Tony Blair Institute for Global Change.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda uliowasilishwa na Mjumbe Maalum ambae pia ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia na Ubunifu nchini Uganda Dkt. Monica Musenero Masanza, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Oktoba, 2021.



No comments:

Post a Comment