LHRC YAZINDUWA RIPOTI YA UTAFITI JUU YA MAKOSA YASIYO NA DHAMANA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 4 October 2021

LHRC YAZINDUWA RIPOTI YA UTAFITI JUU YA MAKOSA YASIYO NA DHAMANA...!

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Sophia Komba (wa kwanza kulia), Mtendaji Mkuu wa LHRC,  Wakili Anna Henga (wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland, Bi. Asma Mshana (katikati) wakizinduwa rasmi ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Sophia Komba (wa kwanza kulia) pamoja na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland, Bi. Asma Mshana (wa pili kulia) na meza kuu wakionesha nakala za ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania mara baada ya kuizinduwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Sophia Komba (wa kwanza kulia), Mtendaji Mkuu wa LHRC, Wakili Anna Henga (wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Finland, Bi. Asma Mshana (katikati) wakizinduwa rasmi ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC), Bi. Sophia Komba akizungumza katika uzinduzi rasmi wa ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 


Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.

Wakili Jeremia Mtobesya akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Wakili Fulgence Massawe akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

Mtendaji Mkuu wa LHRC,  Wakili Anna Henga akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kimezinduwa ripoti maalum ya utafiti wa makosa yasiyo na dhamana nchini Tanzania ikiwa ni jitihada za kuzishauri mamlaka za kisheria na Serikali kwa ujumla kuangalia uhuru wa dhamana kwa mshtakiwa yeyote.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha LHRC, Bi. Sophia Komba alisema utafiti unaonesha katika nyakati za hivi karibuni, haswa miaka mitano iliyopita, Tanzania Bara imekuwa na idadi kubwa ya mahabusu hali inayochangiwa na watuhumiwa wengi kukosa zamana wakati mashauri yao yakiendelea. 

"Idadi hii imetokana na uhalisia kuwa watuhumiwa wengi walishtakiwa kwa makosa ambayo hayana dhamana au makosa ya uhujumu uchumi ambao uhuru wao uliminywa kwa kutolewa kwa cheti cha pingamizi la dhamana cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Wakati watuhumiwa wengi wanabaki kizuizini wakisubiri uchuguzi na upelelezi wa kesi zao kukamilika, ili taratibu zingine kufuata. Kwa wastani inachukua miaka miwili hadi mitatu kwa shitaka kuanza kusikilizwa chini ya kivuli cha kisheria kuwa upepelezi haujakamilika," alisema mjumbe huyo wa Bodi. 

Bi. Komba aliongeza kuwa watu wengi wamekamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa makosa yasiyodhaminika, . Haki hii imepelekea watu wengi kujikuta wakiingia kwenye kwenye ulazima wa kukiri makosa "Plea bargaining" na kulipa fedha ili kupata uhuru wao uliopokwa na kuwepo kwa makosa yasiyokuwa na dhamana kabisa.

"Ni ukweli kwamba kwa miaka mingi Sheria yetu ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura ya 20 [R.E 2019] inaunda nafasi ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini kiholela kwani inaruhusu mtu kukamatwa kwa tuhuma tu jambo ambalo linaweza kutumika vibaya. Endapo mtu atashukiwa tu, basi anakamatwa na kuwekwa kizuizini, hii ni hatari sana kwa nchi ya kidemokrasia kama yetu. Inapaswa kueleweka kwamba, Dhamana ni haki ya kikatiba nchini Tanzania," alieleza mjumbe huyo wa Bodi ya LHRC.

 Aidha aliongeza kuwa Ibara ya 13 (6) (b) na 15 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyorekebishwa, inabainisha dhana ya mtu kutokuwa na hatia na haki ya uhuru na Mahakama inapaswa kuingilia kati katika kuamua swala la dhamana na kulinda haki za watuhumiwa.

"Makosa haya yasiyo dhaminika, ni uonevu mkubwa uliohalalishwa kisheria, kuzuia dhamana sio jambo la kufurahia hata kidogo kwani ni kuwatendea washtakiwa kama wafungwa. Ni muhimu kujua kuwa kumweka mtu kizuizini kuna majukumu makubwa mawili mosi, kuhakikisha mtuhumiwa anakuwepo na kuhudhuria mahakamani pindi kesi yake ikitajwa, na pili, kulinda usalama wa mtu huyo na jamii. Mahakama inapaswa kulinda haki hii kwa wivu mkubwa. Uhuru binafsi na kupewa dhamana, ni vya thamani sana kwenye mfumo wetu wa kikatiba wa "presumption of innocence " unaotambuliwa chini ya kifungu cha 13(6)(b) na ni mhimu sana kuzingatiwa. 

Mwandishi na mhanga wa makosa yasiyo na dhamana B. Kerik, kwenye kitabu chake cha From Jailer to Jailed: My Journey from Correction and Police Commissioner to Inmate. Anaandika kuwa:-"In a free and democratic society such as ours, justice should not eternally abrogate one’s rights to freedom and liberty, except in the most extreme cases." Ikiwa na maana kwamba:-"Katika jamii iliyo huru na ya kidemokrasia kama yetu, haki haipaswi kufutilia mbali haki za mtu za uhuru na utu, isipokuwa katika hali mbaya zaidi.

"Mahakama inapaswa kuingilia kati katika kuamua swala la dhamana na kulinda haki za watuhumiwa. Pindi mtu atakapo  thibitisha atakuwepo mahakamani anapohitajika, na kuweza kupokea adhabu atakapo hukumiwa basi apewe dhamana..." alisema Bi. Sophia Komba.

"Tunapozungumzia swala la dhamana ni mhimu watu kujua kuwa:-Kwa takriban miongo minne (4), kati ya 1945 na 1985, maswala ya jinai  Tanganyika, na baadaye Tanzania Bara, yalitawaliwa na Kanuni ya Makosa ya Jinai. Dhamana ilikuwa moja kati ya mambo mengi yaliyooneshwa chini ya Kanuni. Kifungu cha 123 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1945, ambayo ilisema kwamba mtu yeyote ambaye atakamatwa na kuzuiliwa bila hati na afisa wa polisi anayesimamia kituo cha polisi, anaweza kuomba aachiliwe mnamo kujitambua kwake mwenyewe au dhamana ya polisi au dhamana ya mahakama kadri kesi itakavyokuwa," alibainisha katika hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment