ZANZIBAR YANG’ARA MBIO FUPI KWENYE TAMASHA LA MICHEZO YA WANAWAKE LA TANZANITE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 19 September 2021

ZANZIBAR YANG’ARA MBIO FUPI KWENYE TAMASHA LA MICHEZO YA WANAWAKE LA TANZANITE

Baadhi ya wakimbiaji wa mbio ndefu kutoka mikoa mbalimbali wakishiriki mashindano ya mbio za mita 1500 kwenye Tamasha la Wanawake la tanzanite, leo Septemba 17, 2021 uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Na John Mapepele, Dsm

ZANZIBAR imeibuka mbabe katika mashindano ya mbio fupi uwanja wa Benjamini Mkapa kwenye maadhimisho yanayoendelea ya Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite leo Septemba 17, 2021ikiwa ni siku ya pili kabla ya kuzinduliwa rasmi kesho na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uratibu wa mbio hizo, Robert Kalyahe amesema Zanzibar imeweza kuwa bingwa kwa mbio za mita mia moja katika nafasi zote tatu ambapo amesema mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo ni Hynes Jolini aliyetumia sekunde 11:62 akifuatiwa na Winfrida Makenji aliyetumia sekunde 11:74 na nafasi ya tatu imekwenda kwa Kazija Hassan aliyetumia sekunde12:45.

Pia Kalyahe amesema katika mbio za mita mia mbili nafasi zote tatu zimenyakuliwa na washindi kutoka Zanzibar ambapo amesema Emma Hossea amenyakua nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 24:82 na nafasi ya pili imechukuliwa na Nasra Abdallah aliyetumia sekunde 25:55 wakati nafasi ya tatu imekwenda kwa Neema Ally aliyetumia sekunde 25:86.

Katika mbio za mita mia nne pia nafasi zote tatu zimechukuliwa na  wachezaji kutoka  zanzibar ambapo mshindi wa kwanza Jane Maiga  ametumia sekunde  56:44 mshindi wa pili Shuema Ally ametumia  sekunde 58:67 wakati Gaudenzia Maneno ameibuka mshindi wa tatu baada ya kutumia sekunde sekunde 60:00 katika mbio hizo.

Katika mbio za mita mia nane, Aisha Lubuva kutoka Mkoa wa Arusha ameibuka Mshindi wa kwanza baada ya kutumia dakika 2:15:44 akifuatiwa na Gaudenzia Maneno kutoka Zanzibar aliyetumia dakika 2:16:32 ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Hamida Nassoro kutoka timu ya JKT aliyetumia dakika 2:17:50 kutoka JKT.

Aidha Kalyahe amesema kwenye mbio za mita 1500, Transfoma Mussa kutoka JKT ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia dakika 4:28:42 na nafasi ya pili ikienda kwa Cesilia Ginoka kutoka JWTZ aliyetumia dakika 4:28:53 na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Regina Deogratius kutoka aliyetumia dakika 4:32:12. 

Wakati huo huo timu ya mpira wa mikono ya JKT imeipamiza timu ya Ngome kwa mabao 24 kwa 12 katika mchuano mkali uliofanyika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa.

No comments:

Post a Comment