ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU CCM AKIWA NEWALA MKOANI MTWARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 18 September 2021

ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU CCM AKIWA NEWALA MKOANI MTWARA

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme akihutubia wakazi wa shina namba 1 Kiuta kata ya Mkunya wilayani Newala mkoa wa Mtwara ikiwa siku ya pili ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 - 2025.

 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme akiangalia nguvu ya maji wakati alipotembelea mradi wa maji Makonde uliopo Newala mkoani Mtwara.

Meneja Mradi wa Maji Makonde Mhandisi Emmanuel Komkom akitoa maelezo ya changamoto za mitambo ya kuvuta maji kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme katika kituo cha kupokelea maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji Mkunya wilayani Newala Mkoa wa Mtwara, ikiwa siku ya pili ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM yenye lengo la kukagua na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025. (Picha na CCM Makao Makuu).

No comments:

Post a Comment