MOHAMED DEWJI "MO" AJIUZULU UENYEKITI WA BODI SIMBA SC - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 29 September 2021

MOHAMED DEWJI "MO" AJIUZULU UENYEKITI WA BODI SIMBA SC

Mohamed Dewji ‘Mo Dewji'
BILIONEA Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’ ametangaza kujiengua na nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya timu ya Simba SC na amesema sasa atabaki kuwa kama mwekezaji pekee kwa umiliki wa hisa asilimia 49 zenye thamani ya takribani Sh. Bilioni 20 ndani ya club hiyo.

Akitangaza uamuzi huo leo, kwa njia ya video aliyojirekodi Mo Dewji amesema kwamba kwa sasa nafasi yake itashikiliwa na aliyekuwa Makamu wake, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’ ambaye anauzoefu wa kutosha wa uongozi ndani ya club hiyo.

"Muda umefika mimi kama Mohamed, tumefanya mkutano tarehe 21 mwezi wa tisa, 2021 na tumekubaliana kwamba mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club,". 

Miongoni mwa sababu zingine ambazo kiongozi huyo amezitaja ni pamoja ya kuwa busy kwa safari nje ya nchi mara kwa mara kutokana na biashara zake huku wakati mwingine akishindwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya bodi kutokana na majukumu ya kibiashara. 

Hata hivyo amesema mbali na kuendelea kuwa mwekezaji ndani ya club hiyo, ataendelea pia kuwa mwanachama na mpenzi wa kweli huku akitoa ushauri na maoni pale atakapo hitajika muda wote.

No comments:

Post a Comment