WANASAYANSI CHIPUKIZI WATAKIWA KUPELEKA UJUZI WAO KWA JAMII - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 24 July 2021

WANASAYANSI CHIPUKIZI WATAKIWA KUPELEKA UJUZI WAO KWA JAMII

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga Mashindano ya Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali yaliyofanyika mkoani hapa jana ambayo yaliandandaliwa na Taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST) akizungumza na wanafunzi hao.


Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali, wakionesha kazi zao kwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko alipotembelea mabanda kwenye mashindano hayo.

Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.

Walimu wakiwa kwenye mashindano hayo.

Washindi wa mashindano hayo wakiwa na vyeti vyao baada ya kukabidhiwa.

Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.

Wanafunzi wakiwa kwenye mashindano hayo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

WANA SAYANSI Chipukizi wametakiwa kupeleka kwa jamii ujuzi walioupata wakiwa shuleni badala ya kuufungia kwenye makabati.

Wito huo unetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati akifunga mashindano ya Wanafunzi  Wanasayansi Chipukizi kutoka Sekondari mbalimbali yaliyofanyika mkoani hapa jana ambayo yaliandandaliwa na Taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST)

"Mambo yote mliyojifunza myaboreshe na muende mkayaoneshe huko mbele ya safari kwamba ninyi mtatatua changamoto za wanasingida na nchi yote kwa ujumla na si vinginevyo," alisema Mwaluko.

Alisema kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ni kuwasomesha hivyo walicho kisoma wanatakiwa wakitafsiri na kuacha dhana ya kutaka kuajiriwa hivyo wajiajiri katika kilimo cha alizeti, vitunguu, korosho na fursa nyingine ambazo wanafunzi hao walizionesha katika mabanda yao.

Alisema kupitia mafunzo hayo wataanza kuonesha ubunifu wao wa kilimo kwa kutumia maji kidogo na kupata mazao badala ya kutumia maji mengi.

" Nakuja kutembelea mashuleni ili nione mambo haya mliyojifunza kama yanafanyika na waomba sana mjitahidi changamoto za mkoa wetu wa Singida ziweze kutatuliwa na ninyi kwa kutumia nafasi nzuri mnazo zipata mkiwa masomoni.

Mwaluko aliwaomba waratibu wa mashindano hao kuongeza shule nyingi zaidi kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo na kuwa ataanzisha mkakati wa Siku ya Sayansi katika kila shule na watakuwa wakishindanishwa baina ya shule mbalimbali mkoani hapa.

Alisema mkakati huo utaanzia ngazi ya mtaa, kata, wilaya hadi mkoa na atakaye fuzu atapatiwa zawadi na kupelekwa kushiriki mashindano  ngazi taifa.

Mwaluko aliwata wanafunzi hao wakiwa darasa kujenga tabia ya kuuliza maswali jambo litakalo waongezea uelewa zaidi badala ya kukaa kimya.

Mratibu wa mashindano hayo Mwalimu Nadhiru Bwikizo alisema awali yalikuwa yakifanyika ngazi ya taifa lakini sasa hivi yanafanyika mikoani na wanaofanya vizuri wanapata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi pamoja na kupatiwa zawaidi.

Alisema mkoa wa Singida kwa mwaka 2012 na 2013 kuna wanafunzi kutoka Shule za Ilongero,.Mughanga, Dkt.Salmin Amour na Kijota walifanikiwa kupata nafasi za masomo nje ya nchi baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ngazi ya Kitaifa.

Wanafunzi Stephen Tesha na Qessar Marsha ambao walipata vyeti baada ya kufanya vizuri katika mashindano hayo walitoa wito kwa wenzao kusoma zaidi masomo ya sayansi kwani yana fursa nyingi  katika maisha hasa wakati huu wa dunia ya sayansi na teknolojia.

No comments:

Post a Comment