TAKRIBANI watu 45 wamefariki dunia kwenye ghasia zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini Afrika Kusini, tangu kujisalimisha kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma wiki iliyopita.
Karibu watu 800 wamekamatwa katika ghasia hizo zilizoanza kama maandamano alhamisi iliyopita kupinga kwenda jela kwa Zuma.
Hata hivyo, waandamanaji waligeuza maandamano hayo na kuwa ghasia mwishoni mwa wiki, wakichoma moto, kufunga barabara kuu na kuvamia na kupora maduka.
Askari wamepelekwa katika maeneo mbalimbali kuongeza nguvu na kusaidiana na Polisi kuzima ghasia hizo. Jacob Zuma Rais wa Zamani wa nchi hiyo alihukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuidharau Mahakama kufuatia kesi yake ya ufisadi.
-BBC
No comments:
Post a Comment