Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (mbele, kulia) akiwahimiza Wataalamu kutoka TCRA kuhusu uboreshaji wa Mifumo ya Huduma za Mawasiliano Nchini. |
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imehimiza uboreshaji wa Mifumo mbali-mbali
ya usimamizi wa huduma za Mawasiliano ili kuhakikisha kunakuwa na Usalama na
Ubora wa Huduma nchini.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea mifumo hiyo
kwenye Taasisi ya Udhibiti, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar
Es salaam, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
(Mb) amesema Wananchi wanatarajia kupata huduma bora zenye usalama.
“Upatikanaji wa huduma Bora, za Uhakika na Salama
nijambo la msingi sana kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na Taifa,” amesema
Mhe. Ndugulile.
Katika ziara hiyo Mhe. Ndugulile alipokelewa na
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri K. Bakari na Menejimenti alipotembelea
mifumo ya udhibiti wa Mawasiliano.
Dkt. Ndugulile aliipongeza TCRA kwa ubunifu wa
kujenga Mifumo Wezeshi kwa huduma mbali-mbali za Mawasiliano Nchini, ambapo
alisema uboreshaji wake ni muhimu sana.
Baadhi ya mifumo aliyotembelea Mhe. Waziri ni Mfumo
wa Usimalizi na Udhibiti wa Masafa ya Redio na Televisheni na Kituo cha
Kuratibu Majanga ya Kimtandao (TZ-CERT). TZ-CERT pia itatoa ushuri wa
kitaalam-namna bora wa kudhibiti na kupambana ya majanga mbalimbali ya Kimtandao
kwa Taasisi na Kampuni mbalimbali hapa Nchini.
Mhe. Waziri pia alitembelea Kituo cha Huduma kwa
Wateja ambapo alihimiza TCRA kuendeza kushirikiana na Taasisi zingine zikiwemo
za Kiudhibiti kama Bank Kuu ya Tanzania (BOT).
No comments:
Post a Comment