RAS MPYA SINGIDA AJIPANGA KUPIGANI ELIMU YA MTOTO WA KIKE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 5 June 2021

RAS MPYA SINGIDA AJIPANGA KUPIGANI ELIMU YA MTOTO WA KIKE

Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kulia ), akimkabidhi kabrasha, Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth Mwaluko katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana mkoani hapa. 
 
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi akizungumza katika hafla ya kukabidhi ofisi iliyofanyika jana mkoani hapa.
 Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth Mwaluko akizungumza wakati akikabidhiwa ofisi mjini hapa.

 Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Singida, Doroth Mwaluko (kushoto) na Aliyekuwa  Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi ambaye ameamishiwa Jijini Mbeya wakisaini nyaraka za makabidhiano ya ofisi.


Wakuu wa  Idara mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi .

makabidhiano ya ofisi  yakiendelea.

Wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi.

Na Mwandishi Wetu, Singida,
  
 Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko  amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Dkt. Angelina Lutambi huku akiahidi kusimamia kidete elimu ya mtoto wa kike .  

Akizungumza jana kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mwaluko pamoja na mambo mengine ameomba ushirikiano kutoka kwa watendaji wote mkoani hapa ili kusukuma kasi ya maendeleo lakini zaidi kuleta ustawi kwenye eneo la elimu na maboresho ndani ya sekta ya afya.

"Kitaaluma mimi ni mwalimu na kipaumbele changu hasa ni masomo ya sayansi natamani na nitasimamia kuhakikisha watoto wa kike wanasoma masomo haya kwa mafanikio makubwa,alisema katibu Tawala na akaongeza;

"Kwenye elimu msitarajie kunidanganya na atakaye kwenda kinyume hatutaelewana," alisema.

Aidha kwenye eneo la afya ameomba kila mtendaji kuwajibika ipasavyo ili matarajio ya wanasingida yazidi kudhihirika kupitia serikali yao inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Lutambi ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Mbeya, pamoja na mambo mengine amemueleza Mwaluko kuwa hali ya uchumi wa Mkoa inaenaendelea kuimarika siku hadi siku.

Hata hivyo ameshauri kuwepo kwa msukumo mkubwa na usimamizi kwenye utekelezaji wa sheria ya fedha za serikali za mitaa hasa kupitia tangazo la serikali namba 286 la April 5, 2019 ambalo lilielekeza asilimia 10 ya fedha za mfuko wa Wanawake, Vijana na wenye ulemavu zitolewe ipavyo.

No comments:

Post a Comment