KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHA LAANI 'MAUAJI' YA MTOTO TABORA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 21 June 2021

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHA LAANI 'MAUAJI' YA MTOTO TABORA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Anna Henga (Wakili)  akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na madai ya tukio hilo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uwajibikaji na Uwezeshaji wa LHRC, Joyce Komanya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Anna Henga (Wakili)  akisisitiza jambo kwa wanahabari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na madai ya tukio hilo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uwajibikaji na Uwezeshaji wa LHRC, Joyce Komanya.

Kaimu mkurugenzi Uchechemuzi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bw. Joseph Oleshangay akizungumza katika mkutano huo na wanahabari oliofanyika ofisi za kituo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uwajibikaji na Uwezeshaji wa LHRC, Bi. Joyce Komanya, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Anna Henga (Wakili).

Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi Uwajibikaji na Uwezeshaji wa LHRC, Bi. Joyce Komanya, akizungumza katika mkutano huo na wanahabari. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Anna Henga (Wakili).

Na Mwandishi Wetu

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani tukio la kuchoma moto yumba ambayo inadaiwa ndani yake kulikuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne (4) linalodaiwa kutokea Juni 16, 2021 katika Kata ya Usinge, mkoani Tabora. 

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Bi. Anna Henga (Wakili) amedai kuwa tukio hilo linadaiwa kutokea mnamo tarehe 16 Mwezi wa Sita (6) mwaka 2021 katika Kijiji cha Kombe, Kitongoji cha Songambele, Kata yaUsinge, Mkoa wa Tabora. 

Alisema kuwa taarifa zinasema kuwa watu wanaodaiwa kutekeleza ukatili huo ni Askari ya Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) wakishirikiana na Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Igagala Namba 5 kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua.

"...Ndugu Wanahabari, taarifa zaidi zinasema kwamba Serikali kupitia Mamlaka za Hifadhi ya Taifa ilitenga eneo la hifadhi ya kijiji ya Ngitiri ambayo inazungukwa na vijiji kadhaa. Wananchi mbao mashamba yao yanapakana na hifadhi hiyo walitakiwa waondoke ili kupisha ardhi iliyotengwa. Taarifa zinasema kuwa mwezi Januari mwaka 2021 wananchi hao waliruhusiwa kulima kwa makubaliano ya kwamba baada ya msimu wa mavuno kuisha walitakiwa kuondoka katika eneo la hifadhi. Alisema Wakili Henga.

Wakili Henga anabainisha kuwa wakati baadhi ya wananchi wakiendelea na mavuno (mpunga) ndipo inadaiwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua alitoa amri ya nyumba za wanakijiji hao kuteketezwa kwa moto ambapo nyumba zaidi ya thelathini ziliteketezwa kwa moto pamoja vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hizo ambapo mtoto aliyekuwepondani ya nyumba moja wapo aliunguzwa na kupoteza maisha. 

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinadai kuwa taarifa za kifo cha mtoto zilimfikia Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, lakini hakuna hatua iliyochukuliwa, zaidi ya Mkuu wa Wilaya kuagiza tena zoezi hilo liendelee kwa vijiji vingine hadi vijiji vyote viishe. 

Wakili Henga alibainisha kuwa Ibaraya 24(1)  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977  inasema kwamba; Kila mtu anayohaki ya kumilikimali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.” Kwa maana hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kaliua amekiuka masharti ya Katiba ya nchi kwa kuagiza kuangamizwa kwa nyumba na mazao ya wananchi kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Kituo kimeitaka Serikali kuchukua hatua kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kuwajibishwa kisheria kutokana na mkosa anayodaiwa kuyafanya kwenye zoezi zima la uchomaji moto nyumba hizo. 

Aidha kimemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Waziri wa Maliasili na Utalii wanafanya ziara kwenye Kata ya Usinge iliyoko Wilayani Kaliua ili kutembelea vijiji vyote na kusikiliza kero za wananchi hao juu ya vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kufanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua ili kupata suluhu ya kudumu.

Wameitaka Wizara ya  TAMISEMI kuhakikisha mipaka ya vijiji vilivyo pakana na ardhi ya hifadhi inawekwa bayana ili wananchi wafahamu mipaka ya vijiji vyao ilipoishia kuepuka hali ya mvutano kati ya wanavijiji na mamlaka zinazoendesha hifadhi hizo.


No comments:

Post a Comment