Mkuu wa Vituo vyote vya Kanisa Halisi la MUNGU BABA akizungumza na Waandishi wa habari katika moja ya matukio kanisani hapo. |
NA DUNSTAN MHILU
KANISA Halisi la MUNGU BABA Makao yake makuu yapo Namanga Tegeta jijini Dar es Salaam pembezoni mwa Barabara ya Bagamoyo upande wa kulia ukitokea Mwenge na Upande wa kushoto ukitokea Bagamoyo kutoka barabarani hadi Kanisa lilipo ni takribani mita 120 limekuwa likishirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Kanisa hilo limekuwa likiunga Mkono Shughuli, sera na maadhimio mbalimbali yanayopitishwa na serikali Kama sehemu ya Jamii Kanisa halikuwa nyuma limeendelea kutoa ushurikiano wake kwa Taifa.
Akizungumza katika Ibada ya kuingia kituo cha Uwaminifu Mkuu wa Kanisa hilo BABA Halisi alisema kwakuwa juzi Kanisa hilo limeingia kituo muhimu kuliko vituo vyote, Taifa, Rais Samia Suluhu, Baraza la Mawaziri, Bunge vyombo vya Dola wakae mkao wa kubarikiwa kwani chanzo HALISI ambaye ni MUNGU BABA mwenyewe alikwisha weka kitu yaani Baraka za kutosha ndani ya Taifa BABA Tanzania.
"Tumekwishavuka ni sherehe kubwa haijapata kutokea ninafuraha mno kanisa kuingia kituo cha uwaminifu, ni kituo ambacho kinakwenda kuleta mabadiriko kwa Taifa, Afrika na Dunia nzima lakini pia hatunabudi kuendelea kumuinua Rais Samia Suluhu Hassani kwa Shukrani, dua na maombi ili MUNGU BABA ambaye ni chanzo amlinde na kumtetea katika majukumu yake ya kila siku"
Kanisa hilo limekuwa likiendesha Ibada na maombi kila iitwapo leo ambapo katika maombi, dua na shukrani hujielekeza ama hulinyenyekeza Taifa kwa MUNGU BABA ili aendelee kulilinda pamoja na viongozi wake akiwemo amiri jeshi Mkuu wa nchi ambaye ni MAMA Samia Suluhu Hassani.
Sanjari na kuliombea Taifa Kanisa limekuwa na mchango Mkubwa kwa Taifa la Tanzania kwani tokea kuanzishwa kwake limefanya mambo kaza wa kaza katika huduma za jamii ikiwemo sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu lakini pia katika kuombea amani ya nchi hii ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote kile.
"Tunayafanya haya si kwamba tunazo sana kwa maana ya fedha laahasha ni kazi ya Kanisa kufanya kazi na serikali ndiyo maana Kanisa linapofanya shughuli yoyote au mradi wowote hatuhitaji kujitangaza maana tunafanya kwa Sauti ya chanzo na jamii ndiyo inayosema Kanisa Halisi limejenga wodi huko Tabora, kituo cha polisi ,limechangia madawati na vifaa vya shule ni jamii siyo makuhani wala mimi kwani ni chanzo mwenyewe, kikubwa tu wenye uwezo na Taasisi nyingine zichangie miradi ya Taifa kwa ajili ya kujiletea maendeleo kwakufanya hivyo tutamuunga mkono Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan" anasema BABA Halisi.
Kanisa hilo limejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki ambako kote lina vituo na kutapakaa duniani kote ambako makuhani wenyewe wanapoiskia Sauti ya Chanzo tu kupitia BABA Halisi hawafanyi ajizi hulianzisha Kanisa.
Ukizungumzia Mahusiano ya Seriakali na Kanisa ni ya kutukuka kwani limeota mizizi kuanzia kwenye shina vitongoji hadi Taifani hakuna mahali ambapo Kanisa lipo hakuna mahusiano mazuri na viongozi wake hivyo hufanya kazi na Taifa na Taifa hufanya kazi na Kanisa Halisi la MUNGU BABA.
Na hii ni kutokana na Kanisa hilo kujikita zaidi katika mafundisho ya Ibada ni uzalishaji na upendo usiobagua na kutojihusisha na masuala ya kisiasa bali hushirikiana na wanasiasa pale Kanisa linapohitaji huduma inayohusiana na siasa lakini pia pale wanasiasa wanapohitaji mchango wa Kanisa hilo kwani Serikali haina dini lakini watu wake wana dini na huapa kwa Msaafu na BIBILIA.
Hata hivyo BABA Halisi anawakaribisha watu wote kutoka Mataifa mbalimbali kwa ajili ya huduma za maombezi, ushauri na kiroho kanisa hilo halina masharti yoyote dini,makabila na Mataifa yote mnakaribishwa poopte nchini utakapofika uliza Kanisa halisi la MUNGU BABA lakini hata mikoani na Mataifani Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika Zambia, DR Congo,Msumbiji na kwingineko kwa Dar es Salaam Makao Makuu yake yapo huko Tegeta Namanga.
No comments:
Post a Comment