Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nasser Mbarouk akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe.Pawel Jablonski wakati alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo katika masuala mbalimbali ya ushirikiano.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe.Pawel Jablonski akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nasser Mbarouk wakati alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma na kufanya mazungumzo katika masuala mbalimbali ya ushirikiano.
NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Poland anayeshughulikia na masuala ya Siasa, Uchumi na Maendeleo kwa nchi za Afrika Mhe.Pawel Jablonski ofisini kwake jijini Dodoma.
Akiongelea kikao hicho Balozi Mbarouk amesema kuwa wamejadiliana juu ya kuimarisha mahusiano yaaliyopo kati ya Tanzania na Poland ikiwa ni pamoja na kuanzisha uwekezaji mpya nchini, kuwezesha wanafunzi na wataalamu wetuu kujifunza na kupata utaalmu hasa katika matibabu ya moyo, masikio, pua na Koo.
“Tumekutana hapa na Mhe naibu Waziri kutoka nchini Poland, tumezungumza na kujadliana juu ya namna bora za kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi zetu , tuna maeneo mengi ambayo tunashirikiana baina ya nchi zetu, lakini pia nimewaomba kuanzisha uwekezaji mpya nchini, ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi za masomo kwa ameneo ya matibabu ya moyo, masikio,pua na koo”, amesema Balozi Mbarouk.
Amesema kuwa wamejadiliana juu ya kuhakikisha ujenzi wa Kiwanda cha matrekta cha Kibaha na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia nafaka na kuongeza kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo utawezesha kukwamua miradi hiyo na hivyo kuikamilisha kama ilivyopangwa
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri huyo ameelezea utayari wa Poland katika kuhakikisha mahusiano kati ya Poland na Tanzania yanaimarika na kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta za elimu, kilimo hasa ikizingatiwa kuwa Poland imeendelea kwa kiasi kikubwa kupitia kilimo.
Amesema Poland iko tayari kuisaidia Tanzania kaatika maeneo ya elimu kwa kutoa nafasi za masomo nchin Poland ikiwa ni pamoja na ufadhili kwa wanafunzii wa Kitanzania, uwepo wa mifumo ya kisasa ya kutolea maji taka, kilimo na maendeleo ya usalama wa chakula.
Naibu Waziri huyo. Mhe. Powel yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchni Poland waliobobea katika maeneo ya teknolojia ya kisasa katika sekta za kibenki (smart teknologies) teknolojia ya kisasa katika sekta ya umeme (smart technologies for electricity sector -smart meter connection and lighting systems) na ulipaji kwa kutumia teknolojia za kisasa (smart payment apps).
Naibu Waziri huyo na timu wanatarajia kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shirika la Umeme nchii (TANESCO) Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Benki za CRDB na NMB na Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF).
Ziara ya naaibu Waziri huyo imefuatia mwaliko uliotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Idara ya Ulaya na Marekani
No comments:
Post a Comment