BENKI ya NMB imekabidhi mabati 200 na vifaa vyengine vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari ya Jambiani, Kusini Unguja. Akizungumza katika hafla ya makabidhianao hayo iliyofanyika skulini hapo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar-es-salam, Donatus Richard alisema wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu.
“Benki ya NMB tumeamua kushirikiana pamoja na Jamii yote inayozunguka eneo la Jambiani kuchangia mabati 200 kwa ajili ya kutatua changamoto ya kuvuja kwa madarasa wakati wa mvua,” alisema Donartus.
Aliongeza kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo hivyo kuna kila sababu kwa watoto kupata mazingira mazuri ya kupata elimu na kusisitiza ndio maana benki ya NMB imeamua kuisaidia skuli hiyo.
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Paje ambae pia ni Waziri wa Kilimo, uvuvi, mifugo na umwagiliaji, Sudi Nahoda ameishukuru benki hiyo kwa msaada huo na kusema utasaidia kutatua changamoto ya kuvuja kwa skuli hiyo.
“Nikuhakikishieni kuwa msaada huu mliotupatia una thamani kubwa na kiuhalisia NMB ni moja kati ya mashirika yanayojali Jamii katika kuleta maendeleo.” Alisema Mhe. Sudi.
Kwa upande wake kaimu mwalimu mkuu wa Skuli ya Jambiani, Haji Haji ameishukuru NMB kwa msaasa huo, amesema kwa muda sasa wamekuwa wakikabiliwa na ubovu wa madarasa ambapo wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo katika vipindi vya mvua.
No comments:
Post a Comment