MSHINDI WA PROMOSHENI YA SOKA KAMPENI YA TIGO AKABIDHIWA ZAWADI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 3 February 2021

MSHINDI WA PROMOSHENI YA SOKA KAMPENI YA TIGO AKABIDHIWA ZAWADI

KAMPUNI ya mawasiliano ya Tigo Tanzania leo imemkabidhi piki piki mshindi aliyeshinda kupitia promosheni yake ya Soka Kampeni inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa wateja wake kote hapa nchini. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo mshindi wa promosheni hiyo Allan Misindi kutoka Jijini Dodoma amesema amekuwa akishiriki promosheni hiyo mara nyingi hadi alipopigiwa simu na Tigo makao makuu kuwa ni mshindi wa promosheni hiyo. 

 "Nimekuwa nikishiriki mara kwa mara na sio mara ya kwanza kushinda nimewahi kushinda milioni moja, lakini bado nikaendelea kushiriki hadi nilipopigiwa simu na Tigo makao makuu kuwa nimeshinda piki piki (boda boda)" amesema.
  Amesema alikuwa na ndoto ya kumiliki piki piki maarufu kama boda boda na sasa imefanikiwa atakwenda kuitumia kama boda boda ili iweze kumuingizia kupato kila siku na kumsaidia kutatua changamoto nyingine. Ameongeza kuwa"nawahimiza vijana wenzangu na watu wote kushiriki promosheni hii tigo sio waongo ukishiriki mara nyingi kweli unashinda , mimi nilikuwa nacheza pesa iliisha naweka tena hadi nimeshinda na leo nakabidhiwa boda boda yangu" amesema Misindi. 

 Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Tigo kanda ya Kaskazini, Said Idd amesema promosheni hiyo inaendelea nchi nzima na kwa Dodoma ni mshindi wa kwanza lakini kwa nchi nzima tayari wameshinda washindi wengi. Amesema kupitia Kampeni hiyo ambayo mteja wa tigo anaweza kushiriki kwa kutuma SMS kwenda 15670 na kuanza kupokea maswali yanayohusiana na soka na akipata anajikusanyia pointi mteja anaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo Piki piki, TV na pesa taslimu.

 "Na mteja anayejipatia maswali mengi au kujikusanyia pointi nyingi anajiweka katika nafasi nzuri ya kujishindia TV, pesa taslimu na piki piki kama huyu anayekabidhiwa leo hapa" amesema.

No comments:

Post a Comment