ZIARA YA RAIS WA ETHIOPIA CHATO-GEITA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 25 January 2021

ZIARA YA RAIS WA ETHIOPIA CHATO-GEITA

 

Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akizungumza na Wanahabari wa Geita baada ya mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari wa mkoa wa Geita mara baada ya mazungumzo yake na Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 25 Januari 2021.




Mmoja wa Msanii wa kikundi cha Ngoma za asili cha Chato akionesha uhodari wake  wa kucheza na nyoka aina ya Chatu wakati wa sherehe za kumpokea Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde Chato mkoani Geita.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika uwanja wa Ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.




Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.



Ndege iliyombeba Rais wa Ethiopia Sahle -Work Zewde ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Geita uliopo Chato leo tarehe 25 Januari 2021.



No comments:

Post a Comment