TUMIENI FURSA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU KUKUZA UCHUMI- KASEKENYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 10 January 2021

TUMIENI FURSA ZA UJENZI WA MIUNDOMBINU KUKUZA UCHUMI- KASEKENYA

Kazi ya ujenzi wa Bandari mpya ya Karema ikiendelea Wilayani Tanganyika, Mkoani Katavi, kukamilika kwa bandari hiyo kutarahisisha shughuli za kibiashara kati ya Bandari ya Karema - Tanzania na Kalemii nchini Kongo DRC.

                                      

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (aliyevaa miwani), akitizama kwa makini mchoro wa majengo katika ujenzi wa Bandari mpya ya Karema unaoendelea Mkoani Katavi.

                                       

Muonekano wa sehemu ya barabara ya Mpanda – Vikonge (km 35), iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani Katavi.



Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando, akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bandari mpya ya Karema unaoendelea, Mkoani Katavi.



Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando, wakati alipokagua ujenzi wa Bandari mpya ya Karema unaoendelea, Mkoani Katavi.



Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi, Mhandisi Martin Mwakabende, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mpanda – Vikonge (km 35), kwa kiwango cha lami, mkoani humo.


Muonekano wa sehemu ya barabara ya Kagwira - Karema (km 112), inayounganisha mji wa Mpanda na Bandari mpya ya Karema, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni, Wilayani Tanganyika, Mkoani Katavi.

No comments:

Post a Comment