MWAMBE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA UWEPO MAFUTA YA KULA NCHINI…! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 26 January 2021

MWAMBE AWAHAKIKISHIA WATANZANIA UWEPO MAFUTA YA KULA NCHINI…!

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akitoa ufafanuzi wa hali ya mafuta nchini huku akiwahakikishia watanzania kuwa hakuna uhaba wa Mafuta ya kula nchini wakati huo akitoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaopandisha bei ya mafuta ya kula nchini na kuhaidi kuwachukulia hatua ya kuwafutia leseni za biashara wafanyabiashara wakubwa wanaopandisha bei nje ya ongezeko la bei ya kawaida, Januari 26, 2021 Jijini Dodoma (Picha na Eliud Rwechungura).

Na Eliud Rwechungura

 

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe amewahakikishia watanzania kuwa hakuna uhaba wa Mafuta ya kula nchini na ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaopandisha bei ya mafuta ya kula nchini na amehaidi kuwachukulia hatua ya kuwafutia leseni za biashara wafanyabiashara wakubwa wanaopandisha bei, nje ya ongezeko la bei ya kawaida. 

 

Mhe. Mwambe ameyasema hayo Januari 26, 2021 Jijini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari wakati akitoa ufafanuzi hali ya mafuta ya kula nchini.

 

“Mafuta yapo isipokuwa bei walizonunulia ni kwamba zimepanda kule nje kwahiyo ndo maana kunakuwa na hilo ongezeko la bei, hatutarajii uhaba wa mafuta ya kula tuachotarajia ni hiyo bei kuongezeka na sio uhaba wa mafuta na kwa wale mawakala wakubwa wauze bei ambazo zitakubalika kiwandani na wakiuza bei kubwa kuliko ambayo kiwanda kimetoa na faida yao kulinga na mwenendo wa soko, mimi nitawafutia leseni za biashara zao pia wafanybiashara wakubwa wanatakiwa kuhakikisha wafanyabiashara wa jumla kuwa bei zao zianendanda na bei zilizotolewa kiwandani na sio kuangalia hitaji wanalitengeneza katika soko”

 

Mhe. Mwambe ameendelea kusisitiza na kuwaagiza Tume ya Ushidani Tanzania (FCC), Mkurugezi wa maendeleo ya biashara na Mkurugezi wa viwanda kufuatilia wafanyabiashara waoongeza bei za mafuta ambazo sio za msingi ili waweze kuchukuliwa hatua kali.

 

“Niweagiza FCC ambao ni Tume ya Ushidani Tanzania waweze kufuatilia kwa kina na kuhakikisha kwamba bei zinakwenda vizuri na hakuna ongezeko ambalo sio la msingi, ongezeko la msingi tunalikubali hilo la ongezeko la bei ya mafuta duniani lakini sio msukumo wa wafanyabiashara”


No comments:

Post a Comment