Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole (wa pili kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Claudia Kitta alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Godfrey Kawacha, Kamishna wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Scholastica Msigwa. na kulia ni Kamishna Msaidizi wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Ayubu Mwambete.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyasa English Medium, Mika Alinanuswe.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Keneth Nsilano.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kyela, Leah Katamba. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Ayubu Mwambete.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akisalimiana na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wa Wilaya ya Mbarali, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Musa Nyagalu.
Kamishna wa Skauti Wilaya ya Kyela, Skauta Scholastica Msigwa, akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Keneth Nsilano.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Skauta Sadock Ntole, akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kyela.
Na Dotto Mwaibale
KAMISHNA wa Chama cha Skauti Tanzania Mkoa wa Mbeya, Sadock Ntole amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea wilaya zote za mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi Ntole alisema lengo la ziara hiyo ilikuwa kukusanya takwimu za skauti kupitia kwa makamishna wa wilaya hizo pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazo fanywa na skauti.
"Hii ni ziara ya kawaida ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na skauti katika maeneo yao kuanzia ngazi ya kundi" alisema Ntole.
Alisema katika ziara hiyo aliweza kukutana na viongozi mbalimbali wa wilaya hizo wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na maafisa elimu kwani wamekuwa wakishirikiana na Skauti katika kutekeleza majukumu yao.
Kamishna Ntole aliwataja baadhi ya viongozi aliyokutana nao na kufanya nao mazungumzo ya kiutendaji kuwa ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Afisa Elimu wa Shule za Msingi na Sekondari ambao walimuomba kuendesha mafunzo kwa walimu, walezi ili kuwajengea uwezo katika kusimamia miongozo na shughuli za kiutendaji katika skauti.
Alisema baada ya kuonana na viongozi hao alifanya ziara katika shule za msingi za Kyela na Nyasa na kuendelea na ziara wilayani Mbarali.
No comments:
Post a Comment