Muonekano wa Daraja la Nyahua lililopo katika barabara ya Nyahua – Chaya (km 85.4), mkoani Tabora ambalo ujenzi wake umekamilika.
Sehemu ya barabara ya Nyahua – Chaya (km 85.4) ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika, mkoani Tabora.
Kazi ya ujenzi wa kingo za Daraja la Kizengi katika barabara ya Nyahua – Chaya (km 85.4), mkoani Tabora ukiendelea.
Amesema kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Tabora – Nyahua – Chaya – Itigi – Manyoni yenye jumla ya urefu wa kilometa 259 kutapunguza urefu wa safari kwa kilometa 191 kwa magari yanayopitia barabara ya Tabora - Nzega - Singida hadi Manyoni na hivyo kuleta tija kwa wasafiri na wasafirishaji wa mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi.
“Hakikisheni sehemu ya kilometa sita zilizobaki kuwekwa lami zinakamilika kabla ya mwezi machi ili kuwezesha wananchi kunufaika na barabara hii”, amesema Mhandisi Kasekenya.
Amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora kuilinda miundombinu ya barabara, madaraja na taa za barabarani ili zidumu kama ilivyokusudiwa.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa mkoa huo umejipanga kuhakikisha unalinda barabara zake na kuziwekea taa sehemu nyingi ili kuongeza usalama na kupendezesha mji huo.
Zaidi ya shilingi bilioni 117 zimetumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua - Chaya ambayo imehusisha ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Nyahua na Kizengi ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu.
Naibu Waziri Kasekenya yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku mbili ya kukagua miundombinu inayoendelea kutekelezwa mkoani humo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment