WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Desemba 19, 2020 amemuagiza Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda kuhakikisha
anapeleka Maafisa Ugani katika Halmashauri sita zinazolima zao la chikichi mkoani
Kigoma ili kuwaongezea maarifa Wakulima wa zao hilo.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha
Tanzania inaokoa zaidi ya bilioni 443 kutokana na kuagiza mafuta ya kula kutoka
nje ya nchi.
“Haiwezekani tukaendelea kutumia
fedha hizo zote kwa kuagiza mafuta wakati tunaweza kulima na kuchaka mafuta ya
mawese hapa hapa nchini; Naendelee kusisitiza, Serikali ya mkoa wa Kigoma iwe mfano
kwa wengine”.
“Tija na uzalishaji wa zao
la chikichi hapa Tanzania ipo chini ukilinganisha na nchi kama Malaysia ambayo
uzalishaji wao umefikia tani 10 kwa hekta moja wakati sisi ni 1.6; Ndugu zangu
lazima tupande miche bora kutoka kwa Taasisi zetu za Majeshi, TARI Kihinga na
Sekta Binafsi ambao wamehamasika na kuotesha miche hiyo”.
“Nakumbuka miaka mitatu
iliyopita, nilihamasisha Halmashauri sita za mkoa wa Kigoma kuanzisha vitalu
vya miche bora pamoja na kuhamasisha Taasisi za Majeshi kama Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) Jeshi la Magereza, Taasisi Binafsi kuanzisha vitalu ili mkakati
wetu wa kuleta mapinduzi ya zao la chikiki, lifanikiwe kwa kuwa miti hii ya
zamani; Tija yake ni ndogo”. Amekaririwa Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ameongeza kuwa,uzalishaji wa michikichi ya zamani ni tani 1.6 kwa hekta moja
wakati miche bora uzalisha kuanzia tani 5 kwa hekta huku ikiendelea kuzalisha kwa
zaidi ya miaka 20.
Pia, ameiagiza Wizara ya
Viwanda na Wizara ya Kilimo kuhakikisha ziboreshe mazingira rafiki kwa Wakulima
wa zao la michikichi nchini na uhakika wa soko.
“Naiagiza Wizara ya Viwanda
na Wizara ya Kilimo kuhakikisha zinakuja na mkakati mzuri wa kuhakikisha
Wakulima wa zao la chikichi pamoja na mazao yake;Wanapata masoko ya uhakika.
Kaeni pamoja na mje na mkakati madhubuti kuhusu upatikanaji wa masoko kwa
Wakulima wa zao la chikichi.” Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Aidha,ameipongeza Taasisi
ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI) kwa kutekeleza agizo la kuanza kutoa mbegu
bora ya zao la chikichi zaidi ya mbegu milioni 4.2 sambamba na Wakala wa Taifa
wa Mbegu za Kilimo (ASA) kwa kuzalisha miche bora ya michikichi zaidi ya
456,252.
Awali, katika hotuba yake aliyoisoma
leo katika ukumbi wa NSSF katika Halmashauri ya kigoma Ujiji,uliowashirikisha
wadau wa zao hilo,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majalwa
Majaliwa amesema hivi sasa mahitaji ya mafuta ya kula nchini ni tani 570,000
kila mwaka wakati uwezo wa nchi kuzalisha ni tani 205,000 sawa na asilimia 36.
Wakatihuohuo Serikali huagiza tani 365,000 sawa na asilimia 64 ya mafuta kutoka
nje ya nchi; Ambapo Serikali hupoteza fedha kiasi cha shilingi Bilioni 443 kila
mwaka.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa,
mazao yanayochangia upatikanaji wa mafuta ya kula nchini ni mazao ya chikichi,
alizeti, karanga, pamba, ufuta na soya; ikumbukwe, zao la chikichi ndio linaongoza kwa kutoa
mafuta ya kula kuliko mazao mengine ya mafuta Duniani.



No comments:
Post a Comment