Meneja Uhusiano wa TTCL, Puyo Nzalayaimisi (kulia) akizungumza katika uzinduzi huo. |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Corporation) na Kampuni yake Tanzu ya T-PESA imeendelea kuwaletea huduma kabambe wateja wake ili waendelee kufurahia mawasiliano katika kipindi hiki cha Msimu wa Sikukuu za kuelekea mwisho wa mwaka 2020, ambapo kwa sasa imekuja na huduma za BANDO TAM TAM PLUS pamoja na huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI yenye bonasi za kutosha.
Akitambulisha ahuduma hizo mpya kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa T Pesa, Bi. Lulu Mkudde alisema kuwa BANDO TAM TAM PLUS linapatikana kupitia wateja wa T-PESA, na pia kwa wateja wote ambao wanatumia huduma ya T-PESA. Amesema katika bando hilo wateja watapata huduma ya Intaneti, Ujumbe Mfupi(SMS) na dakika za kutosha kwa siku, wiki na mwezi na pia Ofa hiyo itapatikana kwa gharama nafuu ZAIDI kuliko kawaida.
"...Kwa shilingi 500 mteja atapata MB 600, dakika 5 kupiga mitandao yote na sms 30 kwa siku, Pia kwa shilingi 1,000 atapata 1.2 GB dakika 10 mitandao yote, sms 50 kwa siku 5 na Shilingi 5,000 atapata 2.2 GB, dakika 20 mitandao yote na sms 300 kwa mwezi. aidi na zaidi, Wateja wetu wanazidi kuneemeka na ofa zaidi katika msimu huu wa Furaha, wateja watakaotuma fedha T-PESA kwenda T-PESA yaani ni BURE tu, hakuna MAKATO," alisema Mkurugenzi wa T Pesa, Bi. Lulu Mkudde.
Aidha, Bi. Mkudde aliongeza kuwa katika msimu huu wa furaha, T-PESA inaendelea kuwa karibu na wateja kwa kuwapatia huduma mpya ya vifurushi ya JISOTI yenye bonasi za kutosha. Kifurushi hiki kitakuwa suluhisho kwa watumiaji wa Intaneti na muda wa maongezi kwa sababu JISOTI inampa mteja uhakika wa kuwa na mawasiliano kila siku.
"...Kwa shilingi 3,000, mteja atapata GB 3 – kwa siku 3, lakini katika GB 3 hizo Mteja atatumia GB 1 kila siku ndani ya siku 3. Pia mteja atapewa bonasi ya MB 300, kwa shilingi 5,000, mteja atapata GB 5 – kwa siku 5, lakini katika GB 5 Mteja atatumia GB 1 kila siku ndani ya siku 5. Pia mteja atapewa bonasi ya MB 500." alisisitiza.
Akizungumzia upande wa muda wa maongezi, Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita alisema kwa shilingi 1,000, mteja atapata Dakika 60 – kwa siku 3, lakini katika Dakika 60 Mteja atatumia dakika 20 kila siku ndani ya 3. Pia mteja atapewa bonasi ya Dakika 10, kwa shilingi 2,000, mteja atapata Dakika 125 – kwa siku 5, lakini katika Dakika hizo 125 mteja atatumia dakika 25 kila siku ndani ya siku 5. Na pia atapata bonasi ya dakika 30.
Alibainisha kuwa bonasi zote zitatumika ndani ya siku pindi mteja atakapojiunga kwa mara ya kwanza na kifurushi husika. Hata hivyo aliongeza huduma za TTCL zinazidi kutoa fursa ya ajira kwa Wananchi kuwa Mawakala na imekuwa kiungo muhimu cha kurahisisha shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara hivyo kutoa wito kwamba wananchi waendelee kurudi nyumbani kwa kutumia huduma za kifedha za T-Pesa zenye manufaa makubwa kwao na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment