NMB kupitia kampeni yake ya ‘MastaBata Siyo Kikawaida’ imewazawadia washindi hao zawadi ikiwamo simu janja, Runinga za kisasa, na Jokofu ambapo kila msindi alipatiwa zawadi zenye thamani ya shilingi Milioni 2.4 kila mmoja.
Akizungumza wakati wa kuwatangaza washindi, Maneja wa Benki hiyo tawi la Mlima City, Irene Masaki alisema dhumuni la kampeni hiyo ni kuwahamasisha wateja kutumia kadi za Mastercard na Mastacard QR kufanya manunuzi ya bidhaa au huduma kupitia mtandaoni.
![]() |
| Balozi wa Benki ya NMB - Nancy Sumari, akimpigia simu mmoja wa washindi wa Mastabata Siyo Kikawaida wakati wa kuchezesha droo ya Mwezi iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam. |
Miongoni mwa wateja walioshinda zawadi hizo ni Happy Luka Pallangyo, Masunga Jasila, Francis Julian na Rose Marealle. Mchakato wa kuwapata washindi hao ulisimamiwa na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kuhahatisha Tanzania - Pendo Mfuru.
Promosheni hiyo ilizinduliwa Novemba, mwaka huu na itamalizika Februari, mwakani. Promosheni hiyo, inahamasisha utimiaji wa NMB Mastacard and Mastacard QR katika kufanya manunuzi bila ya kutumia pesa taslimu. Kila wiki na mwisho wa mwezi kuna droo zinafanyika na wateja kuendelea kishinda Zawadi mbalimbali. Wateja wanapaswa kufanya miamala yao kupitia kadi ya NMB Mastercard au QR mara nyingi wawezavyo ili kuongeza nafasi zaidi za kushinda.
Katika kipindi chote cha kampeni, NMB itakabidhi zawadi kwa washindi 40 watakaoshinda Sh. 100,000 kila wiki na washindi 12 watazawadiwa simu janja aina ya Samsung galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. milioni 2.4 kila mwezi.



No comments:
Post a Comment