| Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akizungumza wakati akifungua Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC jijini Dar. |
| Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga akizungumza wakati akifungua Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC jijini Dar. |
| Mtendaji Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi NCC, Dkt. Matiko Samson Mturi akizungumza kwenye Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC lilichofanyika jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NCC
wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Arch. Elius
Mwakalinga kwenye kikao hicho. |
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NCC
wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Arch. Elius
Mwakalinga kwenye kikao hicho. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),
Arch. Elius Mwakalinga akifurahia jambo na menejimenti ya Baraza la Wafanyakazi
la NCC. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi),
Arch. Elius Mwakalinga katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la
Wafanyakazi wa NCC jijini Dar es Salaam. |
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Arch. Elius Mwakalinga amewata Menejimenti na Watumishi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kutangaza kazi wanazozifanya ili zieleweke kwa jamii na kuongeza wigo mpana wa kuwahudumia wananchi.
Akizungumza
leo wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza la Wafanyakazi wa NCC
jijini Dar, Arch. Mwakalinga amesema huu ni wakati wa Baraza hilo kushirikiana
na taasisi nyingine katika sekta ya ujenzi ili kuboresha huduma za ujenzi na
kufanya gharama za ujenzi nchini kuwa za bei nafuu.
“…Hakikisheni
gharama za ujenzi nchini zinakuwa nafuu na zinazotekelezeka ili kuvutia watu
kuwekeza katika ujenzi kwa kuwaelimisha fursa zilizopo na kutatua migogoro ya
ujenzi kwa wakati,” amesema Arch. Mwakalinga.
Aidha
amemtaka Mtendaji Mkuu wa NCC, Dkt. Matiko Samson Mturi kuhakikisha watumishi
waliopo katika baraza hilo wanakuwa na elimu, ujuzi na umahiri ili tafiti
zinazofanywa ziweze kuwa na tija kwa taifa kwa muda mrefu.
“..Hakikisheni
kuwa hamuwi wanyonge kwa kuwaendeleza kitaaluma watumishi wenu, kutangaza kazi
kubwa mnazozifanya ili jamii izifahamu na kunufaika nazo na kufanya tafiti
zinazoleta unafuu wa maisha kwa jamii ikiwemo kutayarisha wataalam wa
ushuluhishi wa masuala ya ujenzi,” amesisitiza Katibu Mkuu, Arch. Mwakalinga.
Naye
Mtendaji Mkuu wa NCC, Dkt. Matiko Mturi amesema kati ya mwaka 2018 hadi 2023
baraza limejipanga kuhakikisha migogoro mingi ya ujenzi inatatuliwa huku wadau
wa ujenzi wakielimishwa ili kuepuka migogoro.
“…Tumejipanga
kuhakikisha tunaboresha idara ya utafiti ili masuala mengi yanayoamuliwa na
baraza hilo yawe ni matokeo ya tafiti za kina, ambayo yatakuwa hayajirudii mara
kwa mara,” amesema Dkt. Mturi.
-Imetolewa na Kitengo cha Habari na
Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

No comments:
Post a Comment